Nafasi Ya Matangazo

October 31, 2012

 
Chocheeni kuni mbichi ugali uive mnacho taka kitokee!! Alikeni mamluki wakija wangojee!! Ni sehemu tu ya kiitiko cha wimbo mpya wa Mkali wa kughani mashairi Tanzania na Afrika Mashariki, Mrisho Mpoto ambao ameupakua na unakwenda kwa jina chocheeni kuni.

Akizungumza na Father Kidevu Blog kwa njia ya mtandao kutoka nchini India ambako amekwenda kwa shughuli maalum za kikazi Mpoto amesema kuwa wimbo huo tayari upo hewani katika Audio na Video.

“Nyimbo hii tayari ipo hewani katika mitandao ya kijamii, na video yake tangu juzi ulinza kusikika duniani kote,’ alisema mpoto.

Mpoto anasema wimbo wake huo amemshirikisha chipukizi Ditto kutoka nyumba ya kukuza vipaji ya THT ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Aidha anasema wimbo huo umefanyiwa kazi na Mwandaaji wa muziki Allani Mapigo.
Miongoni mwa mistari il;iyopo katika wimbo huo wa Nguli huyo ni pamoja na

“watanzania mwendakwao siku zote haogopi giza”
“acheni nirudi nyumbani safari imenishinda, naurizenu ntarudisha”
“mtu anaitapiga nyongo yake anailamba tebna anaagaliwa?”
“nisawa na tawi kavu linapoanguka watu wakapiga kelele…Ahyaaaah!!”
“Katika misimu mmne kwa mwaka tuongeze msimu mwingine wa tano wa kijivusha”
“Raha ya jamvi siku zote ni viraka viraka,na dungu linamficha mlinzi wa ndege wakati wa mvua tuu”
“Eti oooh! Imenyesha juzi juzi tu maji sio mengi nisubirini kule, ilishindikana vipi kuyapima maji kwa mti ““ndio mkwaambia watu wavuke?”
“Mjomba! Binadamu ni sawa na ganda la kitabu mpaka umfungue maandishi ndio uweze kumuelewa”
“Eti lililotokea mbali tufanye limepirta na haliwezi kumzuru mwingine”
“inayotaka kunyesha huwa haisubiri mawingu”
“mimi sidhani kama kujiponya kwa mambo mazito kunahitaji cheti kilichogongwa muhuri wa m,oto au mtaalam wa magonjwa ya akili”
Zaidi ya kutumia neon sahau tu, unawaulizaje watu magogo ya nini wakati unasema kuna nyoka?
Mjomba wewe si uliwapaka wanja…ngoja wao wakupake pilipili halafu kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga”

Mrisho Mpoto aliyezaliwa miaka 34 iliyopita na kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa juzi ni msanii wa muziki wa dansi, filamu, mwongozaji, ngonjela, mshairi, na sanaa ya ngoma kutoka nchini Tanzania.

Anafahamika sana kwa jina lake la utani kama Mjomba au Mpoto. Pia, ametamba sana kwa nyimbo zake zilizogusa hisia za watu kama Salam Zangu Mjomba na Nikipata Nauli aliyoimba na Banana Zorro.
 
Posted by MROKI On Wednesday, October 31, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo