Nafasi Ya Matangazo

October 13, 2012

RPC Mwanza Liberatus Barlow
KAMANDA WA  WA MKOA WA MWANZA SACP LIBERTUS BARLOW (pichani) AMEUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WANAOHISIWA KUWA NI MAJAMBAZI  KATIKA ENEO LA KITANGILI JIJINI HUMO  USIKU WA KUAMKIA LEO.

HABARI ZINASEMA MAREHEMU ALIUWAWA MAJIRA YA SAA TISA USIKU AKIWA NJIANI KUELKEA NYUMBANI KWAKE AKITOKEA KUMRUDISHA DADA YAKE  BAADA YA KUHUDHURIA  KIKAO CHA HARUSI.

MKUU WA POLISI AFANDE  IGP, SAIDI MWEMA AMETHIBITISHA TUKIO HILO NA TAYARI MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI WA JESHI HILO (DCI) ROBERT MANUMBA AKIWA NA KIKOSI CHA MAKACHERO WAMEELEKEA MWANZA KUONGEZA NGUVU KATIKA UPELELEZI MKALI AMBAO UMESHAANZA.

HABARI ZAIDI ZINAKUSANYWA NA TUTAKULETEA KWA KINA BAADA YA MUDA SI MREFU.
Posted by MROKI On Saturday, October 13, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo