Grace Kingalame wa timu ya mpira wa Netiboli Wizara ya Habari, akiudhibiti mpira mbele ya mpizani wake
Timu
ya Habari ikisherehekea ushindi wake dhidi ya Tamisemi katika michuano
ya SHIMIWI inayoendelea katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Habri
walishinda kwa bao 15-14
Kikosi cha wachezaji wa Netiboli cha Tamisemi kabla ya kuanza mchezo wao na Habari.
Kocha
wa Timu ya Netiboli ya Habari , Anna Kibira ( kushoto) akiwa na kikosi
chake kabla ya kucheza na Tamisemi, Habari ilishinda mabao 15-14
Patashika kati ya Ardhi ( bluu) dhidi ya Kilimo.
Ardhi walishinda mabao 30-22.
TIMU
ya mpira wa netiboli ya Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na
Michezo, imeanza vyema katika michuano ya Shirikishio la Michezo ya
Wizara na Idara za Serikali yanayoendelea Mkoani hapa baada ya kuifunga
timu ya Tamisemi mabao 15-14.
Mchezo
huo ambao ulikuwa ni wa vute ni kuvute, kila timu ilipania iwezekuibuka
na ushindi , lakini wachezaji wa timu ya Habari chini ya Kocha Mkuu ,
Anna Kibira, walisimama imara kuhakikisha wanapata ushindi muhimu katika
mchezo huo wa kwanza.
Hadi
mapumziko , Habari ilikuwa mbele kwa mabao 9-7 na kipindi wachezaji wa
pande zote walionesha umahiri wa mchezo huo na hadi mwishi wa mchezo
Habari iliibuka mshindi kwa mabao hayo.
Wachezaji
mahiri wa Habari, Watende Nassor (GA), Grace Kingalame (GS) na Joyce
Kunambi (WD) walitumia uzoefu wao ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi
kwenye mchezo huo muhimu uliofanyika juzi ( Sept 24) uwanja wa Jamhuri
wa Mjini hapa.
Timu
nyingine zilizocheza na kupata ushindi katika michezo hiyo ni pamoja na
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyoibuka na ushindi dhidi ya Mambo
ya Ndani kwa kuifunga mabao 32-13, wakati Ras Mtwara iliifunga Viwanda
mabao 30-17, nyota wa Mtwaraa katika mchezo huo walikuwa ni Halima
Mndolwa na Rehema Mpai.
Mchezo
mwingine iliokuwa ni wa vuta ni kuvute ni kati ya Kilimo na Ardhi,
ambapo vijana wa Ardhi waliibuna na ushindi wa mabao 30-22, mchezaji
Mariam Kungulilo (GS) aliweza kufunga mabao 17 ,wakati mwenzake Kalova
Kihwele akipachika mabao 13, ambapo Madini waliifunga Utumishi mabao
28-20 , wakati Ras Singida iliwafunga Mambo ya Nje mabao 49-11.
MCHEZO WA SOKA
TIMU
sita za soka ikiwemo ua Idara ya Uhamiaji pamoja na Ikulu,
zimewezekufanya vizuri katika mashindano ya michezo ya Wizara na Idara
za Serikali ( SHIMIWI) baada ya kuwagaragaza wapindani wao .
Michezo
hiyo ya makundi tofauti ilifanyika juzi ( Sept 23) katika uwanja wa
Jamhuri wa Mjini hapa, ambapo timu ya Uhamiaji iliweza kuifunga Viwanda
bao 5-2 , wakati Ikulu iliifunga Mambo ya Ndani bao 4-1 .
Pia
katika kinyang’anyiro hicho, Ras Dar es Salaam, iliishinda Wizara ya
Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makzai kwa bao 3-0, Tamisemi kuifunga
Ras Arusha bao 1-0 , Osha kuichakaza Wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika kwa bao 2-0.
Timu
nyingine za soka zilizopata ushindi siku hiyo ni Mahakama kuifunga Ras
Kagera bao 1-0, Idara ya Utafiti wa madini ( GST) nayo kuifunga Mambo ya
Nje bao 1-0 na Hazina kuifunga kwa mbinde timu ya Wizara ya Habari ,
Vijana , Utamaduni na Michezo kwa bao 1-0.
KUVUTA KAMBA WANAWAKE NA WANAUME.
TIMU
tisa za Kuvuta kamba kati ya hizo sita za wanaume na tatu za wanawake
zimefanyavyema katika michezo yao ya kuvuka kamba iliyofanyika juzi
kwenye Uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa.
Kwa
upande wa wanaume, timu zilizopata ushindi ni Maliasili
iliyoishinda Ukaguzi, Hazina kwa kuwatambia TMAA, Uhamiaji iliwavuta
wenzao wa Polisi,Makamu wa Rais ( VPO), iliitoa jasho timu ya GST ,
ambapo Mahakama iliifungia kazi timu ya Haki za Binadamu.
Hata
hivyo , tim nyingine zilizoshinda kwenye kinyang’anyiro hicho ni
pamoja kwa wanaume ni vijana wa Ikulu waliowashinda wenzao wa Tume ya
Sheria.
Kwa
upande wa wanawake, Ofisi ya Bunge iliibuka washindi dhidi ya Ras
Singida, Ofisi ya Waziri Mkuu iliishinda Afrika Mashariki, Afya
iliitambia Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo , Ukaguzi
iliizima Ujenzi , GST ilipata ushindi dhidi ya VPO.
Timu
nyingine za kuvuta kamba wanawake zilizojipatia ushindi ni Viwanza kwa
kuishinda Kilimo, Mifugo kuifunga Mambo ya Nje , wakati vijana wa Hazina
walitoka sare ya Ras Iringa.
0 comments:
Post a Comment