Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo,(kushoto) na Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Raymond Wigenge.
***
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa(TFDA, Haiiti Sillo amesema kwamba kamati maalum inayoaandaa rasimu za awali ya mifumo wa kuoanisha usajili wa dawa katika nchi za Afrika Mashariki(EAC) imeshaanza kazi hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika kipindi cha miaka miwili ijao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa Ushirikiano wa wafanyabiashara wa kutoka nchini China na Tanzania kuhusiana na kampuni hizo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dares Salaam.
Mkutano huo wenye lengo la kutoa elimu kwa wanaotaka wafanyabiashara hao kutoka nchini China wanaotaka kuwekeza katika sekta hiyo.
“Nchi za EAC zinategemee dawa nyingi kutoka nje . Rasimu hiyo itasaidia kuongeza ushirikiano wa kudhibiti dawa bandia kwa pamoja,” . utaratibu huu utakuwa na msharti yanayofanana katika nchi zote ,alisema Sillo.
Alisema mifumo hiyo itasaidia kupunguza gharama za usajili wa dawa na kuwezesha wananchi kupata dawa zilizo bora na uhakika.
Sillo aliwataka waombaji wa kusajili kampuni za utengenezaji dawa na vifaa tiba kuaandaa maelezo yanayotosheleza katika kukidhi viwango vya ubora na usalama wa bidhaa hizo ili kuepusha ucheweleshaji wa usajili huo.
“ Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni waombaji wa usajili wa kampuni hizo kutokidhi viwango vya ubora na usalama wa bidhaa hizi. Hivyo ninapenda kuchukua nafasi hii kuwataka waombaji wahakikishe kuwa kabla ya kuwasisilisha maombi ya usajili wahahakikishe maelezo yao yanajitosheleza,” alisema.
Alizitaja changamoto nyingine ni kuwa kutokuwepo kwa watafiti wa kutosha kutathimini ubora na usalama wa dawa , hata hivyo alisema suala hilo wanalifanyia kazi ili kuongeza rasilimali watu ya kutosha. Changamoto nyingine ni kutokuwepo kwa ripoti za kuonyesha dawa zilizoleta matatizo kwa watumiaji kutoka kwa watoa huduma za afya na watengenezaji wa dawa hizo.
Awali akifungua mkutano huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Regina Kikuli Sillo aliwataka wafanyabiashara hao kuunda mtandao utakaowasaidia kubadilishana uzoefu katika sekta hiyo.
Naye Makamu wa Rais wa Chama cha wafanyabiashara wa uingizaji na usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka nchini China, Meng Dongping alisema wanatengeneza bidhaa hizo ambazo ni bora na kwa gharama nafuu ukilinganisha na nchi nyingine zilizoendelea.
Aliongeza kuwa Tanzania ni nchi ya 11 katika ushirikiano wa kibiashara wa bidhaa hizo barani Afrika na nchi ya pili kwenye soko la bidhaa hizo kwa upande wa nchi za EAC.
Makamu Rais huyo aliongeza kuwa, katika kipindi cha miezi sita cha mwaka 2012 ukuaji wa soko bidhaa hizo nchini Tanzania ,umefikia dola za Marekani milioni 32.61 sawa na asilimia 47 .
0 comments:
Post a Comment