Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Sumbawanga leo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiwasalimu wananchi wa Mkoa wa Rukwa waliojitokeza katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga kwa ajili ya kuupokea mwenge wa uhuru ambao umemaliza mbio zake Mkoani Kigoma na kuwasili Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufanya mbio zake katika Wilaya tatu za Sumbawanga, Kalambo na Nkasi kwa muda wa siku nne.
Kiongozi wa mwenge kitaifa mwaka 2012 Kapteni Honest Ernest Mwanossa akiwa na wenzake pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakifanya maandalizi ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Rukwa kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Samson Mashalla, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi na RPC wakishuhudia mapokezi hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mathew Sedoyyeka akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya tayari kwa kuanza mbio zake katika wilaya hiyo ambapo baadae utaenda Wilaya ya Kalambo na kumalizia katika Wilaya ya Nkasi.
Viongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa wakiwa na viongozi wa Wilaya ya Sumbawanga wakikimbiza mwenge katika moja ya barabara za Manispaa hiyo ikiwa ni kuunga Mkono na kukagua mradi wa Sumbawanga Ng'ara ambao lengo lake kuu ni kudumisha usafi katika Mji wa Sumbawanga. Mradi huo umeasisiwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya na kuzinduliwa rasmi na Mhe. Makamu wa Rais Mohammed Gharib Billal alipokuwa ziarani Mkoani Rukwa.Picha Zaidi http://rukwareview.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment