Nafasi Ya Matangazo

September 06, 2012



UNAPOKUWA na jina kubwa katika jamii basi kupata usumbufu kutoka kwa jinsia tofauti na yako ni kitu cha kawaida kiasi cha kuwa kero katika maisha yako ya kila siku.

Usumbufu huo unamkuta msanii wa maigizo na muziki anayeigiza katika kundi la Ze Comedy linalorusha vipindi vyake kupitia televisheni ya EATV, Rodgers Richard Msemo ambaye anafahamika zaidi kama Masawe Mtata hadi kufikia uamuzi wa kujitoa katika mitandao ya kijamii ili kuwakimbia wasichana ambao humsumbua kumuomba urafiki wa kimapenzi.

Masawe Mtata ambaye alianza kazi ya sanaa ya uigizaji kabla ya kugeukia muziki anasema: “Dah katika vitu ambavyo naviona mzigo katika maisha ya ustaa ni kusumbuliwa na wanawake. Nimelazimika kujitoa kwa mara kadhaa katika facebook baada ya kupata kero kila nikifungua tu.

“Huwa nawaambia (wanawake wanaomtaka kimapenzi) nina mke na mtoto lakini hawataki kusikia, imefikia hatua ya kuwa na akaunti tatu (za facebook) lakini haitoshi hadi nimeamua kukaa pembeni kabisa.

Nashangaa sijui wametoka wapi kwani kabla ya kuanza kuonekana kwenye televisheni na kuimba sikuwaona kabisa.” Masawe Mtata ambaye ni mume wa Rhoda Thomas Kihinja aliyemzalia mtoto wa kike aitwaye Lydia, kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Uongo Kweli, unaotamba katika vituo vya redio na televisheni ndani na nje ya nchini, aliamua kujikita katika muziki baada ya kuvutiwa na rapa wa Mashujaa Musica, Yanick Noha ‘Sauti ya Radi’.
 
Pamoja na kutamba kupitia uigizaji wa komedi, Masawe Mtata  anatarajiakukamilisha albamu yake itakayokuwa na nyimbo 10 katika mtindo wake aliouita ‘Bongo Techno’ ambapo ndani yake kuna mitindo ya dansi,
taarab, mdundiko, bongo fleva na dancehall.

Msanii huyo ambaye ni mchaga halisi tayari ameshakamilisha nyimbo tano ambazo ni Uongo Kweli, Sebene, Niremberembe (Nibembeleze), Nipe Kidogo Nichangamshe Damu na Pampalila, lakini bado hajaipa jina albamu yake
hiyo hadi atakapokamilisha nyimbo zote.

Masawe Mtata ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto sita ya Mzee Richard Msemo na Elaisi Minja, alianza kazi ya sanaa ya uigizaji katika kundi la Kidedea miaka ya 2000 kabla ya kugeukia muziki ambapo alitengeneza albamu mbili ambazo hazikufanya vizuri na ndipo alipojiingiza kwenye kampuni ya promosheni ya Intergrated akiwa kama mcheza show na MC kabla ya kurudi tena katika uigizaji.

MASAWE MTATA ANADHAMINIWA NA MTANDAO WA www.sufianimafoto.blogspot.com
Posted by MROKI On Thursday, September 06, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo