Nafasi Ya Matangazo

August 24, 2012


Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini,Mh Dr Msengi akikabidhi sehemu ya msaada kwa muwakilishi wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira cha Amani Center kilichopo nje ya mji wa Moshi,kwa mratibu wa kazi za kijamii Japhary Salum,Msaada huo umetolewa jioni ya leo na kampuni ya Clouds Media Group,ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kuisaidia jamii.
Baadhi ya Watoto wa kituo cha Amani Center wakishuhudia tukio hilo,ambalo pia limewahusisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya,akiwamo Juma Nature,Joe Makini,Bob Junior,Shetta,Ferouzi,Lina na wengineo ambao pia watatumbuiza usiku wa leo kwenye tamasha la Serengeti   Fiesta 2012,kwenye uwanja wa chuo cha Ushirika.
 Pichani anaezungumza nia Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini,Mh Dr Msengi akizungumza kwa ufupi ikiwemo sambamba na kuishukuru kampuni ya Clouds Media Group iliombatana na baadhi ya wasanii,kwa namna ambavyo wamekuwa wakiijali jamii kwa namna moja ama nyingine,shoto ni Mratibu wa shughuli hiyo kutoka Clouds,Simon Simalenga na mwisho shoto ni mratibu wa kazi za kijamii Japhary Salum pamoja na Afisa Ustawi wa jamii wa Moshi,Bwa. Sammy Mulemba.
Mratibu wa shughuli hiyo kutoka Clouds,Simon Simalenga akimkaribisha Mkuu wa Wilaya na wageni wengine waalikwa mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva,kwenye moja ya darasa la kituo hicho cha Amani Center.
Ofisa Mawasiliano wa kituo cha Amani Center,Salima  Khatibu akitoa maelezo na historia fupi ya kituo hicho kwa baadhi ya wasanii walioshirikiana na kampuni ya Clouds Media Group kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo hicho jioni ya leo.
Ofisa Mawasiliano wa kituo cha Amani Center,Salima  Khatibu akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Moshi mjini,Mh.Dr Msengi alipowasili kwenye kituo hicho kwa niaba ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula.
Pichani ni baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo na wasanii mbalimbali waliojitokeza kushirikiana na kampuni ya Clouds Media Group kutoa msaada huo.
Posted by MROKI On Friday, August 24, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo