Nafasi Ya Matangazo

July 24, 2012


Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam leo imekubali kichapo cha goli 3-1 kutoka kwa wapinzani wao wa sasa Azam ambao ni washindi wa pili wa Ligi Kuu, katika mchezo wao wan ne wa Robo fainali ya kombe la Kagame 2012.

Azam kwa ushindi huo sasa imetinga nusu fainali na kwa soka la uhakika walilotandaza hii leo wanamatumaini makubwa wa kunyakua Kombe hilo kwa mara ya kwanza iwapo itafanikiwa kuingia fainali kwa kuifunga AS Vita kutoka Burundi.

Mbali na Azam na Vita timu nyingine zitakazo chuano katika Nusu fainali ni Yanga na APR .

Magoli ya Azam leo yalipachikwa kiamini na Mpachika Mabao namba moja wa Ligi Kuu John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyepachika wavuni magoli hayo huku moja kipindi cha kwanza na mawili katika kipindi cha pili.

Bocco alipachika goli la kwanza dakika ya 17 na kupachika mengine mawili katika dakika ya 46 na msumari wa mwisho dakika ya 73.

Goli la Simba lilifungwa na Shomari Kapombe aliyetokea nyuma na kupeleka mashambuzi langoni mwa Azam na kuzaa matunda.

Vikosi vya leo ni kama hivi

Azam FC; Deo Munishi, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Michael Balou/Ramadhan Chombo, Kipre Herman Tcheche/George Odhiambo ‘Blackberry’, Salum Abubakar, John Bocco, Ibrahim Mwaipopo na Khamis Mcha ‘Vialli’/Jabir Aziz.

Simba SC; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Shomary Kapombe, Lino Masombo, Juma Nyosso, Mussa Mudde, Uhuru Suleiman/Kiggi Makassy, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Jonas Mkude/Amri Kiemba. 
Posted by MROKI On Tuesday, July 24, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo