Kaseja akishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa wa Urafiki Cup |
KIPA namba moja wa Tanzania, anaechezea Mabingwa wa Soka Tanzania Bara na Mabingwa wapya wa Urafiki, Juma Kaseja amezidi kujidhihirisha kuwa yeye ni tishia katika kudaka mikwaju ya penati baada ya kudaka penati mbili kati ya 5 za Azam na kuisaidia klabu yake ya Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Urafiki baada ya kushinda kwa penati 3-1 katika mechi yao ya fainali iliyoamuliwa kwa ‘matuta’ kufuatia sare ya 2-2 katika muda wa kawaida kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo usiku.
Kaseja ambaye pia ni nahodha wa Simba, alidaka kiufundi penati za Waziri na Mwaipopo huku Himid Mao akipaisha na hivyo kuipa Simba ubingwa wa michuano hiyo ikiwa ni siku moja tu kabla ya kuanza kampeni yao ya kuwania taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).
Mwinyi Kazimoto, Amir Maftah na Kigi Makassy ndio waliofunga penati za Simba huku Haruna Moshi ‘Boban’ akikosa baada ya penati yake kugonga ‘besela’, wakati aliyefunga bao la Azam akiwa ni Khamis Mcha pekee.
Katika dakika 90 za kwanza, Simba mabao yao kupitia Felix Sunzu na Mwinyi Kazimoto aliyefunga kwa penati huku mabao ya Azam yakiwekwa wavuni na Mcha Khamis na John Bocco.
Kwa ushindi huo, Simba walizawadiwa kombe na fedha taslim Sh. milioni 10 wakati Azam walizawadiwa Sh. milioni 5.
Vikosi:
Simba: Juma Kaseja, Shomari Kapombe/Haruna Shamte (dk.45), Amir Maftah, Mungusa, Juma Nyoso, Mussa Mudde/Haruna Moshi ‘Boban, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Salim Kinje/Uhuru Selemani(dk.61), Felix Sunzu/Kigi Makassy (dk.74) na Abdallah Juma/Danny Mrwanda (dk.45).
Azam: Deogratias Munishi, Ibrahim Shikanda, Waziri Juma, Said Moradi, Joseph Owino/Agrey Morris (dk.45), Ibrahim Mwaipopo, Kipre Bolou/Jabir Aziz (dk.66), Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Kipre Tchetche/John Bocco (dk.45), George Odhiambo na Khamis Mcha.
0 comments:
Post a Comment