Meneja mkuu wa shirika la ndege la Fly540 bw. Brown Francis kushoto akizungumza katika mkutano navyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana katika wakati akiomba radhi kwa wateja wake kutokana na tatizo lilitokea wiki iliopita na kupelekea abiria wake kuchelewa katika safari yao baada ya ndege waliokuwa wasafiri nayo kupata itilafu .kulia ni Meneja wa masoko wa kampuni hiyo Bi .Jean Uku.
*********
Five Forty Aviation Ltd,Kampuni ya ndege ya fly540 inayofanya safari zake hapa Tanzania imeeleza kusikitishwa kwake na taarifa zisizokua rasmi zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini. Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja mkuu wa compuni hiyo hapa nchi bw. Brown Francis amesema alipokea taarifa hizo kwa mstuko na mshangao mkubwa kwani kwa upande mmoja hazikuwa na ukweli ndani yake.
“Ndege yetu ilipata hitilafu kwenye injini jumamosi mchana mara tu baada ya kutua Mwanza, kama ilivyo kawaida yetu mafundi wetu wakaanza kuirekebisha lakini katika hali ya kusikitisha, jitihada za mafundi hazikufanikiwa kutokana kuharibika kwa kifaa ambayo haikuweza kupatikana mara moja na badala yake ilibidi ikanunuliwe huko Nairobi nchini Kenya.” Alisema Francis
Aliongeza kuwa kutokana kutopatikana kwa kifaa hicho kwa hara kampunib hiyo kwa kufata sera zake zenye kumjali mteja kwanza, iliingia gharama ya kuwalipia wwateja wake matumizi yote hoteli wakati inasubiri ndege nyingine kutoka kwa washirika wake ambayo kwa bahati mbaya haikua karibu na hivyo kulazimika kusubiri kuliko kusafirisha abiria wake kwa ndege mbovu kwa kuhofia usalama wa wateja wake ambapo ililazimika kukodi ndege ndogo iliyokwenda Kenya kuchukua kifaa kilichoharibia ambacho kesho yake asubuhi kilianza kufungwa na kukamilika majira ya saa nane mchana.
Taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari zilitokana kutokuelewa kwa baadhi ya wateja na wasafiri wa ndege hiyo kutokana kwamba walitakiwa kusubiri hadi uongozi wa ndege hiyo fly540 watakapo waambia ndege iko tayari au ndege hakuna, hata hivyo hakukua na mtu yeyote kati yao au mwandishi yeyote aliyepiga simu kwa uongozo husika ili kupata ufafanuzi juu ya swala hilo.
Kwa niaba ya kampuni ya Fly540 limited, uongonzi na wafanyakazi wote , Meneja mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw Brown Francis amechukua fursa hiyo kuitaka radhi umma ya watanzania wenye mapenzi mema na kampuni hiyo pamoja na wateja wake wote waliopatwa na tatizo hilo na kuwataka wasamehe na kusahau kwani uongozi na wafanyakazi wa kampuni hiyo wanawahakikishia kutotoakea kwa tatizo kama hilo tena.
“Kwa niaba ya kampuni yetu tunatambua umuhimu na unyeti wa tatizo hili kibiashara, tunatambua umuhimu wateja wetu, tunatambua umuhimu wa watanzania kwa ujumla,hivyo fly 540 tunaomba radhi sana kwa yale yaliojitokeza na tunaahidi kutokubali hali kama ile itokee tena, tunawapenda sana wateja wetu na tunawahiji katika safari zetu kwani bila nyinyi sisi pia sio kitu.
Ndege moja ya kampuni hiyo ipo katika matengenezo ya kubadilishwa injini ambapo mara baada ya kukamilika fly540 itatangaza ruti mpaya hapa Tanzania
0 comments:
Post a Comment