Nafasi Ya Matangazo

May 27, 2012

Gari la Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bishop Dickoson Maganga lililochomwa moto usiku wa jana katika eneo la Kariakoo nje ya kanisa hilo ambapo uharibifu wote unaelezwa kuwa umegharimu shilingi millioni 120.


Askofu wa Madhehebu ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Kariakoo, Dickson Kaganga amesema watu wasiojulikana wamechoma moto jengo la Kanisa hilo jana usiku majira ya saa 3.30 usiku na kusababisha hasara kubwa.

Amesema mnamo saa hizo, watu wasiojulikana walivamia Kanisa hilo huku wakitoa lugha chafu zenye kuashiria uvunjifu wa amani, ambapo walinzi wa Kanisa hilo ilibidi wajifiche kuokoa maisha yao.

Amefahamisha kuwa vitu vilivyoungua ni pamoja na gari dogo aina ya Corrola, Viti vya plastiki, Vyombo vya muziki, Kuta za kanisa pamoja na Vifaa vingine.

Askofu Kaganga amefahamisha, Jengo la Kanisa nalo halifai kwamatumizi ya sala na linahitaji matengenezo makubwa ikiwemo viungio vya umeme kwani hadi sasa hawajaweza kufanya tathmini kujua hasara kamili iliyopatikana.

Ameongeza kuwa, wahalifu hao waliofanya vitendo vya kuchoma moto Kanisa hilo, walidhamiria kufanya mauaji kwani zana walizokuwa nazo ni visu, mawe na silaha nyingine za kienyeji.

Amesema kuwa, aliwaelekeza walinzi wa Kanisa hilo kujificha katika sehemu ambayo isingekuwa rahisi kuonekana kutokana na nyimbo za maneno waliyokuwa wakisema yaliashiria kabisa kufanya uhalifu mkubwa.

Askofu Kaganga ameiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuviangalia kwa makini vikundi vyenye kuashiria shari ili kuitunza na kuienzi amani ya Taifa hili.

 Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) liliopo mtaa wa Kariakoo mjini Unguja limechomwa moto jana usiku wa kuamkia leo.

Katibu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Sheikh Abdallah Said Ali ambaye ni miongoni mwa wanaotafutwa na jeshi la polisi akizungumza na Radio DW asubuhi mapema kabla ya taarifa ya kutafutwa kwao kutolewa kwa vyombo vya habari (picha zote kwa hisani ya  Salma Said).Na Salma Said, DW, Zanzibar/zanzibaryetu.wordpress.com.

*******
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU

(JUMIKI)

للجنة الدعوة الإسلامية

THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION

P. O. BOX: 1266 -Tel:             +255-777-419473 begin_of_the_skype_highlighting            +255-777-419473      end_of_the_skype_highlighting       / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com

MKUNAZINI ZANZIBAR


Tarehe 27MAY2012 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W) na Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), ahli zake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu.

Jumuia ya UAMSHO inatoa taarifa rasmi kwa umma wa Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kwamba haihusiki na vitendo vyote vya uvunjaji wa amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Kama alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila kwa haki ya Uislamu (maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukmu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa, Mahekalu na n.k) zisivunjwe wala zisiharibiwe.

Jumuia inatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Jumuiya inayachukulia matukio yaliyotokea usiku wa jana, na yanayoendelea tangu alfajiri leo, kama ni njama za makusudi za wale wasioipendelea amani nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao.

Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za wengine.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.

WABILLLAH TAWFIQ .
Posted by MROKI On Sunday, May 27, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo