Zaidi ya
wafanyakazi 40 wa Malaka ya Bandandari Tanzania, (TPA) walifanya ziara ya
kuhamasisha Utalii wa ndani nchini kwa kutembelea Hifabdhi za Manyara, Serengeti na
Ngorongoro. Sehemu ya wafanyakazi hao ilikuwa ni wafanyakazi Bora wa mwaka 2012
ambao walipataka kutoka idara mbalimbali za Mamlaka hiyo nchini, hivyo TPA
kuamua kuwapa Motisha ya kutembelea vivutio hivyo vya Utalii nchini na kujionea
mambo mbalimbali ya maajabu ya wanyama yaliyopo katika hifandhi hizo hasa ya
Bonde la Ngorongoro.
Mashirika na
taasisi nyingine nchini hazina budi kuiga mfano huu na si kuwapeleka watumishi
wao bora nje ya nchi badala yake wawapeleke katika hifadhi zetu na kuhamasisha
utalii wa ndani.
Baadhi ya
Wafanyakazi Bora wakifurahia jambo wakati wa mapumziko katika hifadhi ya
Serengeti.
Simba Jike
akikata kiu ndani ya bonde la Ngorongoro.
Baadhi ya
Wafanyakazi wakimsikiliza mhifadhi wa Bonde la Oldupai Gorge (hayupo pichani)
wakati akitoa maelezo kuhusu historia ya bonde hilo.
Mojawapo ya
hoteli za kitalii walipofikia Wafanyakazi Bora wa TPA.
Maafisa wa TPA, Janeth
Ruzangi (kushoto) na Jones Macha (kulia) katika mapumziko baada ya safari ndefu
mbugani.
Mwenyekiti wa
DOWUTA Bandari ya Dar es Salaam Bw. Athman Mkangara (kushoto) na Mwenyekiti wa
DOWUTA Makao Makuu, Samuli Chala (kulia) wakiteta jambo.
Ndege huyu
alikuwa rafiki wa kila mtu katika mbuga ya Serengeti.
Pundamilia wanasifika kwa kila mmoja kuwa na mistari
ambayo haifanani katika ngozi zao
Simba akiwa hoi
muda mfupi baada ya kuwinda Nyati katika Mbuga ya Serengeti.
Burudani ya ngoma ya Kimasai
TPA mpo juu hongereni sana mmedumisha utalii wa ndani Big Up
ReplyDelete