Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda (pili kulia) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni Vumbua Hazina chini ya Kizibo inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia zake za Tusker Lager, Plisner Lager na Serengeti Lager, kulia ni Meneja wa Bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo ,kulia ni Bw. Mrisho kutoka shirika la Bahati Nasibu ya Taifa na kushoto ni muwakilishi kutoka kampuni ya PWC,Tumainiel Malisa
Meneja wa Bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni Vumbua Hazina chini ya Kizibo inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia zake za Tusker Lager, Plisner Lager na Serengeti Lager, kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Serebgeti (SBL) Teddy Mapunda,pamoja na Bw. Mrisho kutoka shirika la Bahati Nasibu ya Taifa na kushoto ni muwakilishi kutoka kampuni ya PWC,Tumainiel Malisa
Pichani ni Wawakilishi kutoka kampuni ya Pricewaterhouse Coopers (PWC),Tumainiel Malisa (shoto) na James Ndetiko (kulia) sambamba na Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Allan Chonjo wakifuatilia kupatikana kwa washindi wawili wa bahati nasibu ya Promosheni Vumbua Hazina chini ya Kizibo
Meneja wa Bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akizungumza na mshindi wa kwanza kwa njia ya simu,kutoka Musoma aitwaye John Gati mwenye umri wa miaka 32,ambaye amejishindia jenereta.
Meneja wa bia ya Tusker Lager,Ritha Mchaki akizungumza na mshindi wa kwanza kwa njia ya simu mbele ya wanahabari na wadau mbalimbali,aitwaye Godfrey Shao mwenye umri wa miaka 24 kutoka jijini Mwanza aliyejinyakulia Bajaj.
======== ========
MSHINDI WA KWANZA WA JENERATA NA BAJAJ APATIKANA!
Ni katika droo ya promosheni ya ‘vumbua hazina chini ya kizibo ’ Mei 2, Dar Es Salaam: Droo ya kwanza kabisa ya promosheni inayoendelea ya kampuni ya bia ya Serengeti Breweries LTD (SBL) inayojulikana kama‘Vumbua hazina chini ya kizibo’ imefanyika leo katika ofisi za kampuni hiyo, maeneo ya Oysterbay jijini Dar Es salaam.
Kampuni ya bia ya Serengeti ni kampuni tanzu ya kampuni ya DIAGEO PLC (UK) ya Uingereza na kupitia bidhaa zake, Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni hii tangu wiki iliyopita. Promosheni hii ya aina yake iliyosheheni zawadi mbalimbali kubwa na ndogo kama vile Jenereta , Pikipiki , Bajaji , Gari na zawadi zingine nyingi zikiwemo pesa taslimu na bia za bure.
Droo hii leo, ilihudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hii, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE na wahakiki na wakaguzi kutoka PriceWaterHouseCoopers (PwC) kuonesha jinsi washindi wote watapatikana kihalali.
Akiongea katika hafla hii, meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager, Bw. Allan Chonjo amesema kwamba “Tayari tumeweza kupata washindi waliopata pesa taslimu na wakafanikiwa kupata pesa zao kupitia MPESA ndani ya masaa 24. Pia, washindi wamepatikana ambao wamejishindia zawadi za vinywaji vilivyopo katika promosheni hii.
Naomba nisisitize, kwamba promosheni hii inalenga kuinua na kubadilisha maisha ya watanzania hususani wateja wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni yetu ikiwa ni sera mojawapo ya kampuni hii kuisaidia jamii kwa njia mbalimbali kupitia bidhaa zake zenye ubora wa kipekee. Pia ningetaka niseme ni njia ya pekee ya kuwashukuru watanzania kwa ushirikiano wao kwetu”.
Mshindi wetu wa droo ya kwanza ni John Gati mwenye umri wa miaka 32 kutoka Musoma ambaye amejishindia jenereta pamoja na Godfrey Shao mwenye umri wa miaka 24 kutoka jijini Mwanza aliyejinyakulia Bajaj.
Baada ya kuchezeshwa droo kwa umakini kabisa na Rita Mchaki -Meneja wa bia ya Tusker Lager alipiga simu kwa washindi na ilikuwa dhahiri kwamba washindi walishtuka na kufurahia ushindi wao. Baada ya maongezi machache, waliweza kujieleza vizuri majina yao kamili na wanapopatikana ili waweze kupatikana siku chache zijazo kwenye hafla fupi ya kuwakabidhi zawadi zao.
MAELEKEZO:
Nunua bia ya Serengeti Premium Lager, Tusker lager au Pilsner Lager na angalia ndani ya gamba jepesi lililo ndani kizibo utapata namba zilizopo katikati ya kizibo, Fungua sehemu ya kutuma ujumbe mfupi kwenye simu yako, nakili namba hizo mfano 259487, kisha tuma kwenda namba 15317. Fanya hivyo kwa kufuata maelekezo katika vipeperushi na magazeti. Pia unaweza kujipatia bia ya bure papo hapo kati ya bia zote tatu zilizoainishwa katika promosheni hii.
0 comments:
Post a Comment