Mwakilishi wa kampuni ya bia ya Serengeti Mkoani Iringa bw. Philip Ghucha (kulia) akikabidhi jenereta kwa mshindi wa promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO Bw. Reymond Denis kutoka Iringa aliyejishindia jenereta hiyo kupitia bia ya Tusker Lager, promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti nchi nzima kwa wiki 16 kupitia bia ya premium Serengeti Lager,Tusker Lager na Pilsner Lager ambapo zaidi ya milioni 180 zinashindaniwa.
Mshindi wa jenereta bw. Reymond Denis(katikati) akielezea hisia zake baada ya kukabidhiwa jenereta ambapo alisema kuwa hakutegemea kuwa atashinda lakini sasa anaamini kujaribu ni kushinda na sasa anaweza kufanya kilimo cha umwagiliagi kwa kutumia genereta hiyo,” naishukuru sana SBL kwa kubadisha maisha yangu na kuwa bora zaidi.
washabiki na wapenzi wa bidhaa za SBL wanywaji wa bia ya Tusker wakimpongeza bw. Reymond Denis ambapo baadaye kila mmoja alipata nafasi ya kutoa maoni na kusema kuwa siku zote waliamini promosheni ni uzushi lakini sasa wamejawa na imani, morali na hamu ya kuendelea kushiriki, “ Kwanza tumefurahi sana SBL kutufuata hadi huku kijijini kwetu kutuletea zawadi kwani tumezoea kampuni zingine wanakuita ifate mwenyewe na wakati mwingine mtu huna hata shilingi moja ya kusafiri wala ya kusafirishia zawadi hiyo, tunawashukuru sana SBL.
0 comments:
Post a Comment