Nafasi Ya Matangazo

May 17, 2012

 Mkuu Mpya wa Wilaya ya Sumbawanga Mathew S. Sedoyeka akila kiapo cha utii mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya leo katika ukumbi wa Ikulu ndogo katika Manispaa ya Sumbawanga baada ya uteuzi wa hivi karibuni wa Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kushika madaraka hayo kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali John Antonyo Mzurikwao. 
 Mhe. Sedoyeka akisaini kiapo hicho mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya.
 Mkuu wa Wilaya mpya ya Kalambo Luteni Edward O. Lenga akila kiapo cha kuiongoza Wilaya hiyo mpya mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mkuu wa Wilaya wa Kwanza wa Wilaya hiyo mpya iliyomegwa kutoka katika Wilaya ya Sumbawanga.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi kitendea kazi Mkuu wa Wilaya mpya ya Kalambo Luteni Edward Lenga ambayo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atayoitumia kama muongozo wa shughuli zake za kila siku awapo madarakani.

 Mkuu mpya wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya leo katika ukumbi wa Ikulu ndogo Mkoani Rukwa. Mkuu huyo wa Wilaya maechukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Joyce Mgana baada ya uteuzi wa hivi karibuni wa Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akisaini hati ya kiapo cha Mhe. Iddi Kimanta baada ya kuwaapisha wakuu wote watatu wa Wilaya za Sumbawanga, Kalambo na Nkasi.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Francis Kilawe akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kutoa neno baada ya kuwaapisha wakuu hao wa Wilaya.

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akihutubia washiriki waliohudhuria hafla hiyo ya kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Rukwa. Katika hotuba yake hiyo alitoa maagizo 16 kwa Wakuu hao wa Wilaya na kuwataka wayafanyie kazi kwani ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazoukabili Mkoa wa Rukwa. Maagizo hayo yanapatikani chini kwenye Hotuba ya Mkuu huyo wa Mkoa.

Hotuba ya Mkuu wa Mkoa iliyokuwa na maagizo 16 kwa Wakuu wa Wilaya waloapishwa. Kuisoma shuka hadi mwisho wa Post hii.

 Mkuu mpya wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akitoa neno lake la salamu katika hafla hiyo. Alisema kuwa kuja kwake Rukwa ni kwa ajili ya kuwatumikia wananchi kwa uwezo wake wote na si vinginevyo. Alitoa kaulimbiu yake mpya ya Wilaya yake ya Nkasi kuwa ni"Nkasi Kasi zaidi". Aliendelea kusema kuwa "Mimi ni kamisaa wa Chama cha CCM ndani ya Wilaya yangu ya Nkasi" Aliahidi kutekeleza itikadi za Chama cha Mapinduzi katika kuleta maendeleo Wilayani humo.


 Iddi Kimanta akihutubia kwenye hafla hiyo baada ya kuapishwa.

 Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mathew S. Sedoyeka akitoa salamu zake mara baada ya kuapishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo baada ya uteuzi wa hivi karibuni wa Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuiongoza Wilaya hiyo. Alisema kuwa hakuja Mkoani Rukwa kufanya biashara bali kuwatumikia wananchi.

 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Luteni Edward O. Lenga akitoa salamu zake baada ya kuapishwa. Aliahidi kuafanya kazi bila maneno mengi.

 Baadhi ya watumishi katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Sunto Mantage(Nyuma) walikuwepo kushudia tukio hilo la kihistoria. Wakwanza kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu katika Sekretarieti ya Mkoa Rukwa Samson Mashalla, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Sumbawanga Mathew S. Sedoyeka.

Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo ya kihistoria ambayo walikuwepo viongozi mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa Dini, wananchi na wagani mbalimbali walioalikwa pamoja na waandishi wa habari.Zaidi Bofya Hapa
Posted by MROKI On Thursday, May 17, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo