BENDI
za Mashujaa na Mashauzi Classic zitatumbuiza kwenye kinyang’anyiro cha
kumtafuta mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2012 kitakachofanyika Juni Mosi
katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.
Akizungumza
jana, mratibu wa shindano hilo, Godfrey Kalinga, alisema kuwa wameamua
kuweka burudani nyingi yenye ladha tofauti ili kukidhi kiu ya rika zote
watakaohudhuria shindano hilo ambalo ni kivutio kwa wakazi jijini.
Kalinga alisema shindano hilo pia litatumika kwa ajili ya kusherehekea miaka 10 tangu kuasisiwa kwa shindano la Miss Tabata.
“Shindano
la mwaka huu litakuwa ni la aina yake kwa sababu hii utakuwa ni mwaka
wetu wa 10 tangua kuanza kuandaa Miss Tabata ndio maana tunaleta
burudani nyingi,” alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen
Arts.
Alisema warembo waliyowahi kushinda mataji mbalimbali ya shindano hilo, pia wamealikwa kusherehekea miaka 10 ya Miss Tabata.
Shindano
hili limedhaminiwa na Dodoma Wine, Redds, Integrated Communications,
Fredito Entertainment, Multichoice Tanzania, Screen Masters, Kitwe
General Traders, Step In Electronics, Brake Point, Atriums Hotel na Lady
Pepeta.
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Dar West Park.
Warembo
hao ni Neema Saleh (18), Noella Michael (19), Queen Issa (20), Hycalisa
Joseph (18), Phillios Lemi (19), Wikllihemina Mvungi (20) na Nightness
Rajab (19).
Wengine
ni Suzanne Pancras (19), Caroline David (21), Khadija Nurdin (19),
Jamila Omary (18), Advent Mamkwe (21), Nadya Marjeby (21), Axer Peter
(20), Rahama Hassan (19), Mercy Mlay (21) na Diana Simon Laizer (20).
Warembo 10 watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Mrembo anayeshikilia taji la Tabata kwa sasa ni Faiza Ally.
Warembo
wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania
ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya
kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds.
Katika shindano la mwaka juzi Juliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.
Juliet ndiye anayeshikilia taji la dunia la Miss Progressive International.
0 comments:
Post a Comment