Wafanyakazi wa waljis, kuanzia kushoto, Bhavisha, Samira, Fatima, Francisca, Farha, Nadia na Munira wakifurahia cheti na trophy.
***********
Mji wa Durban unaosifika kuwa na vivutio mbalimbali ikiwa pamoja na fukwe zenye mandhari ya kuvutia watalii wengi, maduka ya kimataifa na migahawa ya kimataifa takribani wiki mbili zilizopita, toka tarehe 12 – 15 Mei, uligubikwa na shamrashamra za kipekee wakati wa maonyesho ya shughuli za utalii na usafirishaji toka duniani kote na hasa barani Afrika, ijulikanayo kama INDABA.
Maonyesho hayo yanayofanyika kila mwaka mwezi Mei nchini Afrika Kusini yamekuwa kivutio kikubwa kwa bidhaa bora za utalii toka barani Afrika, na huvutia wageni wa kimataifa kutoka sekta ya usafiri na utalii na vyombo vya habari kutoka duniani kote. INDABA inamilikiwa na shirika la Utalii la Afrika Kusini na kuendeshwa na kampuni ya Witch & Wizard Creative (Pty) Ltd.
Watangazaji wa huduma mbalimbali za usafirishaji na utalii ikiwa pamoja na wageni waliofika kutembelea mabanda mbalimbali wakati wa sherehe hizi wanakisiwa kuwa ni karibu watu elfu tatu ambao walibadilisha sura ya mji wa Durban ambao ni maarufu kwa shughuli za utalii katika jimbo la Kwa Zulu Natal nchini Afrika Kusini.
Nao Wafanyabiashara katika sekta ya utalii kutoka Tanzania waliokuwa wakishiriki katika maonyesho hayo mjini Durban nchini Afrika Kusini wameeleza kuridhishwa kwao na tija iliyopatikana kwa kushiriki kwao katika maonesho hayo ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kuanzisha mahusiano na wafanyabiashara wenzao katika sekta hiyo kutoka nchi mbalimbali duniani.
Makampuni yapatayo 55 ya kusafirisha watalii na yale yanayotoa huduma za utalii ya Tanzania yalishiriki katika maonyesho haya, hii ikiwa pamoja na makampuni 49 toka sekta binafsi na 6 kutoka mashirika ya serikali, wakiongozwa na Bodi ya Utalii Tanzania, walishiriki katika tukio la siku nne uliofanyika katika katika ukumbi wa Albert Luthuli Convention Centre (Durban ICC), kulingana na maelezo ya afisa habari mwandamizi wa Bodi ya Utalii, ndugu Geoffrey Tengeneza.
Miongoni mwa shamrashamra katika maonyesho hayo kampuni ya Waljis Travel Bureau Ltd ya jijini Dar es Salaam, ilihudhuria maonyesho hayo kupitia moja kampuni yake tanzu ya Karibu Holidays na kutunukiwa tuzo ya “Wakala bora katika Afrika Mashariki na Mashariki ya Kati" ya mwaka 2011/2 iliyotolewa na shirika la ndege la Afrika ya Kusini (South African Airways).
Tuzo hiyo ilitolewa katika mkutano mkubwa wa wajumbe zaidi ya 400 wa ngazi ya juu, ambao ni pamoja na mabalozi na wakurugenzi watendaji kutoka sekta ya usafiri na utalii. Ndugu Susai Nathan, Meneja maendeleo ya biashara wa Karibu Holidays alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya kampuni ya Waljis Travel Bureau.
Ndugu Nathani ni mmoja wa maelfu ya watu wanaofanya kazi katika sekta ya utalii ambaye ni shehemu ya jitihada kubwa zilizoiwezesha kampuni yake kushinda tuzo hii. Tuzo hii, kulingana na ndugu Susai, inaonyesha mambo mawili makubwa, kwanza kwamba mtiririko wa biashara kati ya Afrika Kusini na Tanzania unakua kwa kasi, akielezea kwamba watu wengi wamekuwa wakisafiri kutoka serikalini, mashirika ya kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali, na hasa sekta ya madini na nishati. Pili, kampuni ya Kitanzania imeweza kutoa viwango vya juu vya huduma zinazohitajika katika soko la kimataifa miongoni mwa wenzao katika nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na kanda ya maendeleo ya Mashariki ya Kati, ikiwa pamoja na Afrika ya Mashariki.
Waljis Travel Bureau Limited ilianzishwa takribani miongo miatano iliyopita jijini Dar es Salaam. Pia ni mwakilishi wa Tanzania wa kampuni ya kimataifa ya usafiri duniani, Carlson Wagonlit Travel (CWT). Kwa mujibu wa ndugu Susai, kampuni yake inafanya kazi kwa karibu sana na mashirika ya kimataifa, vyombo vya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi, katika kuhakikisha mipango ya usafiri imeratibiwa vyema katika viwango vya kimataifa na pia kuto msaada wakati na baada ya huduma.
Waljis si kampuni ya kawaida ya kuratibu huduma za usafiri tu bali, Susai anasema, "Kampuni yetu si ya kuuza tiketi tu, bali tunaenda mbele zaidi kuzingatia mtindo wa ongezeko la thamani ya wateja katika maeneo mbalimbali kama hoteli, usafiri, vibali vya kuingia nchi (visa), na kuwapa wateja msaada unaohitajika katika uwanja wa ndege wanaposafiri. Na hii inatufanya sisi kuwa kampuni yenye upekee katika huduma hizi kulingana na uzoefu wetu”.
Zainab Dhalla, Mkurugenzi Mtendaji, wa kampuni ya Waljis Travel Bureau anasema ilikuwa fahari ya kampuni yake Waljis Travel na Tanzania kwa kupokea tuzo hiyo, na kwamba wanajielekeza katika kuendelea kuboresha na kuongeza viwango vya huduma, na kujenga huduma ya mtandao (portal on-line) kwa ajili ya kufuatilia mipango ya usafiri wa wateja wao. Miongoni mwa mipango mahsusi ya kampuni yao ni kuhamia katika ofisi kubwa itakayokuwa karibu na jingo la ubalozi wa India, Kinondoni jijini Dar es Salaam katika miezi miwili ijayo.
Waljis Travel Bureau kwa sasa ofisi zao zinapatikana kati ya mtaa wa Zanaki na Indira Gandhi mkabala na Habib African Bank. Karibu Holidays (moja ya kampuni tanzu yake) inalenga katika huduma za burudani, ikiwa ni pamoja na safari mbalimbali ikiwa pamoja na safari za fukwe, Dar es Salaam, Zanzibar na duniani kote.
Kwa wenye sherehe mbalimbali za harusi, na usafiri wa aina ya kipekee wa majini ‘safari Cruise’ kutembelea visiwa kama vile Mbudya na Bongoyo, ambavyo vipo karibu na jiji la Dar es Salam, unaweza kuratibiwa na kampuni hii. Kadhalika kuna mashua na aina mbalimbali za usafiri ambazo hutumika kusafirisha wageni, ikiwa pamoja na helikopta, ambayo inaweza kutumika kwa ajili ya dharura, uhamisho, safari maalumu, uokoaji na kupeleka wagonjwa.
Kampuni ya Waljis inapatikana Zanaki na Indhira Ghandi Street na kwenye runinga www.waljistravel.co.tz barua pepe travel@waljis.co.tz simu 0784 780 332 masaa 24.
0 comments:
Post a Comment