Nafasi Ya Matangazo

May 22, 2012

Dini ya hindu kupitia dhebhebu la shri swaminaraya imeahidi kutoa elimu kwa waumini wake pamoja wananchi wasio wahumini kuhusiana na sensa ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kufanyika mapema mwezi agosti.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini arussha leo,Ofisa Uhusiano wa dhehebu hilo Kaushik Vasan alisema kuwa dini yao ipo tayari kutoa ushauri kwa waumini wao pamoja na wananchi kwa ujumla ili kuweza kubaini nini maana ya sensa ambapo pia watawahamasisha wananchi hao kushiriki zoezi hilo siku hiyo.

Alisema kuwa pia kwa kutumia sherehe za uzinduzi wa jengo la msikiti wao ambao wameujenga jijini hapa ambao wanatarajia kuzindua leo watahamasisha watu wote ambao watahudhulia sherehe hizo kushiriki zoezi hilo.

Vasan alisea kuwa kutokana na umuhimu wa sensa hiyo ya watu na makazi wataisaida serikali katika kuhamasisha waumini wake na wakazi wa jiji hili kwa ujumla juu ya umuhimu wa kujiandikisha wakati wa sensa.

Akiongelea uzinduzi wa msikiti huo alisema kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Ghanshyam Charan Swami ambaye ni mmoja wa wasaidizi wa kiongozi wao,mkuu wa dini hiyo ambaye ni HDH,Pramukh Swami Maharaj (91) aishiye nchini India.

Alibainisha kuwa katika uzinduzi huo wanatarajia zaidi ya wageni 800 kutoka nje ya nchi ambao watafika kusherekea pamoja zoezi hilo ,huku akibainisha kuwa mbali na masuala ya kiimani  wanajikita pia katika kusaidia jamii ikiwepo kupanda miti kwa ajili ya mazingira ,kutoa huduma mbalimbali za kijamii kama vile kusaidia hospitali mbalimbali vifaa ,pamoja na kuwasomesha watoto yatima na wale ambao wanaishi katika mazingira hatarishi.
Posted by MROKI On Tuesday, May 22, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo