Nafasi Ya Matangazo

May 22, 2012

Rais mpya wa Shirikishio la Riadha Tanzania ( RT), Antony Mtaka ambaye ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro ( aliyesimama ) akitoa hotuba yake ya shukrani kwa wajumbe wa Shirikisho hilo, Viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi ( wapili kutoka kushoto) kwa kumchangua kwa kura za kishindo pamoja na safu yake ya uongozi mpya baada ya kushinda mpinzani wake Kanali Mstaafu Juma Ikangaa , uchaguzi huo ulifanyika juzi (Mei 20) Mjini Morogoro.
Rais mpya wa Shirikishio la Riadha Tanzania ( RT), Antony Mtaka ambaye ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro ( aliyeshika ua) akipongezwa na baadhi ya wajumbe waliochaguliwa wa Shirikisho hilo juzi ( Mei 20) wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Mjini Morogoro ( aliyekaa kulia) ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa ( BMT) Dioniz Malinzi.
Rais mpya wa Shirikishio la Riadha Tanzania ( RT), Antony Mtaka ambaye ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro akipongezana na aliyekuwa mgombea mwenzake kwenye nafasi hiyo, Kanali mstaafu Juma Ikangaa ( wenye suti ) baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu na washindi wa nafasi mbalimbali kupatikana , uchaguzi huo ulifanyika juzi ( Mei 20) Mjini Morogoro.
Kanali Mstaafu Juma Ikangaa ( wa kwanza kulia) akifuatilia matangazo ya matokeao ya uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania ( RT) uliofanyika Mei 20, mwaka huu mjini Morogoro, Ikangaa aligombea nafasi ya Rais wa RT na kushindwa dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka .
KATIBU MKUU WA RT, SULEIMAN NYAMBUI NA TABASAMU LA USHINDI.
Posted by MROKI On Tuesday, May 22, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo