
Waimbaji wa nyimbo za Injili wakiwasili ndani ya uwanja wa Taifa jioni hii,kutumbuiza tamasha la pasaka 2012,kulia ni Christina Shusho,Upendo Kilahilo pamoja na Upendo Nkone wakiwa na watoto wao.

Mwanamuziki nyota wa muziki wa nyimbo za nchini kutoka Afrika Kusini,kati pichani akiwasili ndani ya uwanja wa Taifa,tayari kutumbuiza tamasha la pasaka jioni ya leo.

Malkia wa nyimbo za injili Rose Muhando akiwasabahi wasahbiki na wapenzi wa muziki wa kiroho alipokuwa akiwasili kwenye uwanja wa Taifa,kutumbuiza tamasha la pasaka.

Mwimbaji nyota wa muziki wa nyimbo za Injili kutoka nchini DRC-Congo Solomoni Mukubwa akiwasili kwenye uwanja wa Taifa jioni hii,huku akiwasalimia wapenzi na washabiki wa muziki wa injili hapa nchini waliofika kwenye tamasha la Pasaka.

Sehemu ya wakazi kutoka sehemu mbalimbali wakiendelea kumiminika kwenye uwanja wa Taifa kusherehekea tamasha la pasaka linaloendelea hivi sasa.

Wakifuatilia kwa makini yanayoendelea hivi sasa hapa Uwanjani,ambapo katika tamasha hilo mgeni rasmi ni Waziri wa mambo ya Nje Mh Bernad Membe.


Maandalizi yakiendelea sehemu ya mafundi mitambo.

Sehemu ya jukwaa ambako wasanii wataonesha umahiri wao wa kuimba na kucheza huku wakimsifu Mungu.


Patanogaje uwanja wa Taifa ile live live leo.
Picha na JIACHIE BLOG
0 comments:
Post a Comment