Na Mwandishi wetu, Tanga TIMU ya soka ya Kijitonyama Veterans imeendelea kutamba katika mechi za kuadhimisha sikukuu ya Pasaka baada ya kuifunga timu ya Middle Eight ya Tanga bao 1-0. Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Disouza, timu zote ziliashambuliana kwa zamu na kukosa nafasi kadhaa za wazi kutokana na washambuliaji kukosa umakini mara walipokuwa wanaingia katika eneo la hatari. Baada ya kusakosa nyingi, Kijitonyama Veterans ilifanikiwa kupata bao la ushindi kupitia kwa Abdallah Salum “Carlos” kwa shuti kali baada ya kuwekewa pande safi na Kiki de Kiki. Bao hilo liliwafanya Middle Eight kuanza kushambulia kwa nguvu, hata hivyo ngome ya Kijitonyama Veterans chini ya Brian Makundi ilikuwa makini kuondoa hatari zote zilizoelekezwa golini kwao. Mchezo huo ulikuwa wa pili kwa Kijitonyama Veterans ambapo katika mchezo wa kwanza dhidi ya timu ya Tolabola, timu hizo zilitoka suluhu. Timu hiyo ilitarajia jana kumaliza ziara ya mechi tatu za sikukuu ya Pasaka mkoai Tanga kwa kupambana na timu ya Mkwakwani veterans inayoundwa na wachezaji nyota wa Tanga waliowahi kuichezea timu ya Taifa na timu za Coastal Union, Yanga na Simba. Mratibu wa timu hiyo, Majuto “Ronaldo de Lima” Omary alisema kuwa japo ni mara ya kwanza kwa timu yake kufanya ziara mkoani Tanga na wanatarajia kufanya ziara kama hiyo katika mikoa mingine nan je ya nchi. “Huu ni mwanzo tu, lakini mipango yetu ni kuweka historia kwa kusafiri mpaka nje ya nchi kwa mechi za kirafiki za kudumisha uhusiano na maveterani wa huko,” alisema Majuto. |
April 08, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment