Nafasi Ya Matangazo

February 06, 2012

Meneja Masoko wa TBL,Mamongae Mahlare,Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelikindo,Jaji Mkuu wa Shindano Safari Lager Nyama Choma,Lawrence Salvi pamoja na mpiga picha wa TBC,Jane John walila nyama choma ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa shindano hilo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imezindua rasmi yale mashindano ya aina yake na ya kuvutia ya kuchoma nyama yajulikanayo kama “Safari Lager Nyama Choma”

Mashindano haya hushirikisha majiko ya baa mbalimbali katika umahiri wa kuchoma nyama na hatimaye zawadi hutolewa kwa washindi.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya mwaka huu, meneja wa Bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema madhumuni makubwa kwa bia ya Safari lager kuendesha mashindano haya ambayo yamekuwa kivutio kwa walaji wa nyama na watumiaji wa bia ni kuhakikisha tunaleta changamoto kwa majiko yanayochoma nyama, ili kuhakikisha walaji wanapata kile kilicho bora kabisa. 

Watumiaji wa bia ya Safari Lager, hupendelea sana kuitumia huku wakisindikiza na nyama choma iliyoandaliwa vizuri, hivyo kupitia mashindano haya, bia ya Safari Lager inaendeleza utamaduni wa kunywa bia na kula nyama. Kufuatia ubora wa hali ya juu wa bia ya Safari lager, tunafurahi sana pale ambapo mnywaji atapata pia nyama iliyo bora ili mtumiaji aweze kuridhika zaidi.

Mashindano ya mwaka huu yatafanyika katika mikoa mitano ambayo ni; Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Arusha,Mbeya.na Mwanza. Kuna ongezeko la mkoa wa Mwanza ambao mwaka juzi haukushiriki. Ni matarajio ya bia ya Safari Lager kuyapeleka mashindano haya katika mikoa yote siku za usoni.

Akitaja zawadi za washindi, Shelukindo alisema; baa itakayoshika nafasi ya kwanza itajinyakulia shilingi Milioni Moja, mshindi wa pili, Laki Nane, Mshindi wa Tatu laki Sita, Nafasi ya Nne; Laki Nne na nafasi ya Tano shilingi Laki Mbili. Zawadi hizi zimegawanywa kwa kila mkoa.

Utaratibu wa kupata baa zitakazoshiriki mashindano haya utaendeshwa kwa njia ya simu, ambapo wananchi watatakiwa kutuma ujumbe mfupi usemao “Safari kisha Mkoa uliopo ikifuatiwa na jina la Baa” kisha tuma kwenda namba 0763 514 514 Utapokea ujumbe kukuhakikishia kuwa kura yako imepokelewa. 

Jopo la majaji litapitia kura zote na Baa ishirini kwa Dar Es Salaam na Kumi kwa mikoa mingine zitakazokuwa zimepata alama za juu zaidi ndizo zitakazopambana katika hatua ya pili ya tano bora ambapo majaji watazitembea tena na kutoa maksi kulingana na vigezo waliovyo navyo kasha baa hizo zitapambana katika eneo la wazi ambapo mandhari ya kula nyama na kunywa bia itakuwa imeandaliwa.

Kwa Upande wake Jaji mkuu wa Mashindano ya mwaka Douglas Sakibu akizungumzia

Vigezo vitakavyoangaliwa na majaji katika mashindano haya ni pamoja na Usafi wa eneo, vifaa na muhusika, uchaguzi wa nyama, maandalizi ya nyama, jinsi ya uchomaji, muda unaotumika, jinsi nyama inavyofikishwa kwa mlaji na Ladha. Baa zitakazofanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro zitapewa semina elekezi juu ya vigezo hivi kabla ya mpambano.

Alisema hii ni fursa ya pekee kwa wachoma nyama na wenye mabaa kuweza kupata mafunzo yakinifu juu ya uandaaji na uchomaji wa nyama toka kwa wataalam wenye ujuzi na waliobobea kwenye taaluma hiyo ili kuweza kukuza na kuboresha biashara zao na hatimae kufikisha kwa wateja kitu kilichokuwa na ubora wa hali ya juu.

Mashindano ya Safari Nyama Choma mwaka huu yanafanyika kwa mara ya nne ambapo mwaka jana washindi wa Jiji la Dar Es Salaam walikuwa Kisuma Bar ya Temeke Mwembe Yanga,Mbeya walikuwa Mbeya Canival,Kilimanjaro walikuwa Makanyaga bar ya Soweto na Arusha walikuwa SongaMbele Bar ya Sakina.
Posted by MROKI On Monday, February 06, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo