Nafasi Ya Matangazo

February 09, 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Februari 9,2.2012. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lymo, Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Hawa Ghasia na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Marina Njelekela.

Waziri Mkuu,Mh.Mizengo Pinda amesema kuwa amewafuta kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Blandina Nyoni pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Deo Mtasiwa kuanzia leo hii kutokana na kuonekana kuwa wao ndio kiini cha mgogoro huo ambao umekuwa ukisababisha matatizo makubwa kwa Taifa.

Waziri Mkuu amewataka Madaktari waunde kamati maalumu ambayo itakusanya mapendekezo ya madaktari wote na kumpelekea yeye ili aweze kuyafanyia kazi,huku akiwataka Madaktari hao kurudi kazini na kuendelea na majukumu yao kama ilivyokuwa hapo awali. 
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayoongoza mgomo wa madaktari, Stephene Ulimboka akiuliza swali wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipozungumza  na madaktari na wauguzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam, Februari 9,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Februari 9,2.2012. Kushoto  ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Hawa Ghasia na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Marina Njelekela.
 Baadhi ya madaktari na wauguzi wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao kwenye Hospitali ya taifa ya Muhimbili, Februari 9, 2012.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayoongoza mgomo wa madaktari, Stephene Ulimboka baada ya kuzungumza na madaktari na wauguzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam, Februari 9,2012.
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya madaktari na wauguzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kuzungumza nao Februari 9, 2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Posted by MROKI On Thursday, February 09, 2012 1 comment

1 comment:

  1. changa la macho hiyo...wacha wakenue meno tu watajuta siku za usoni!

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo