Nafasi Ya Matangazo

February 03, 2012

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeukabidhi mkoa wa Mara tani za saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mkoani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimnisho ya miaka 35 ya CCM.

Saruji hiyo itatumika kujenga madarasa kwa ajili ya wanafunzi ambao wameshindwa kuanza kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa madarasa licha ya kufaulu mwaka huu.

Akikabidhi mifuko hiyo kwa mkuu wa mkoa huo, John Tupa, Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema saruji hiyo imetolewa na makada wa CCM ambao wameamua kutoa mchango huo kwa kupitia CCM ikiwa ni kuunga mkono maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM.

Nape alisema makada hao ni Zulfikar Nanji wa Kampuni ya  Mwanza Huduma Ltd (mifuko 400) Joseph 'Msukuma' Kasheku  mfanyabiashara ambaye pia Diwani wa Kata ya Nzela, Geita na Mjumbe wa NEC, Vedastus Mathayo ambao wote wametoa mifuko 100 kila mmoja.

Alisema kada mwingine ni Dk. Isack Chacha Ng'ariba ambaye aliahidi kutoa tani 200 za saruji ahadi ambayo aliitoa papo hapo wakati wa makabidhiano hayo.

Nape aliwashukuru wafanyabiashara makada hao wa CCM kwa kuiunga mkono CCM katika kuhakikisha kwamba sherehe za miaka 35 ya CCM inakuwa na mafanikio makubwa kwa kutekeleza azma ya kuchangia shughuli za maendeleo.

Alisema, wafanyabiashara na makada hao wanaichangia CCM pia kama kuonyesha shukurani yao kwa kuweza kufanya biashara zao kwa miaka mingi katika mazingira ya amani na utulivu chini ya uongozi wa serikali ya CCM.

"Mkiona vinaelea vimeundwa, amani na utulivu huu uliopo ni mazingira yaliyojngwa na kuendelea kutunzwa na CCM tangu ilipoanza kutawala nchi hii baada ya kurithi uongozi kutoka vyama vya TANU NA ASP miaka 35 iliyopita", alisema Nape.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa mkoa alisema, jumla ya watoto  6486 kati ya asilimia 50.3 ya watoto waliofaulu, wameshindwa kuanza kidato cha kwanza mkoani mwake kutokana uhaba wa vyumba vya madarasa licha ya kufaulu.

Mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa unahitaji madarasa 718 wakati yaliyopo ni 479 na hiyo kuwa na upungufu wa madawati 239 na kwamba wilaya ya Bunda ndiyo inayoongoza kuwa upungufu wa madarasa.

Alisema licha ya kupata msaada huo wa saruji bado mkoa unahitaji mabati, mbao na madawati kwa ajili ya madarasa yatakayojengwa.
Posted by MROKI On Friday, February 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo