Timu ya Villa Squad Fc mchana huu inataarajia kuingiaa Bungeni mjini hapa kwa mwaliko maalum wa Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan ambae ni mdau na rafaiki wa timu hiyo.
Villa wapo wamjini humo kwa siku ya pili leo toka walipowasili mapema jana na kuingiaa mafichoni kwa ajili ya maasimu wao, Polisi Dodom, mchezo utaakaocheza uwanja wa Jamhuri hiyo kesho Jumamosi Feb 11.
Ofisa Habari wa Villa, Andrew Chaale alisema wachezaji na viongozi watapaata muda wa kuona shughuli mbalimbali za Bunge kisha baadae wataendelea na majukumu yao kama kawaida ikiwemo mazoezi.
Villa wanataraajia kuingia uwanjani huku wakiwa na haali ya furaaha baaada ya kushinda michezo yaao miwili ya awali ikiwemo kuwafunga Toto Africa ya Mwanza na Simba Sc,. hivi karibuni na kufikishaa pointi 13.
___________________________________________________________________________
WAKATI HUO HUO TIMU ya Villa Squad Fc ‘Kambimoto’ kesho inashuka dimbani kukipiga na Polisi Dodoma, ya mjini hapa katika uwanja wa Jamhuri.
Villa imeingia iliwasili mjini hapa mapema juzi na kufikia mafichoni kwa kujiwinda na maasimu wao hao ambao mchezo wa mzunguko wa kwanza walilala goli 2-1, uwanja wa Chamazi.
Akizungunza kwa njia ya simu, Ofisa habari wa Villa, Andrew Chale alisema timu hiyo iliwasili salama mjini Dodoma ikiwa kwenye msafara wa watu 27, ukijumuisha viongozi na wachezaji.
“Timu imefika salama Dodoma, hikiwa chini ya mkuu wa msafara, Idd Mbonde na imejichimbia sehemu maalum huku ikijiwinda kwa mchezo huu muhimu dhidi ya Polisi Dodoma” alisema Chale.
Kwa upande wake, kocha wa timu hiyo, Habibu Kondo alisisitizia nidhamu na akili kwenye mchezo ndio silaha ya ushindi. “Dhana iliyojengeka ya vurugu na utovu wa nidhamu kwa wachezaji wangu kwa kkupewa kadi za njano na nyekundu, sasa basi kwani tayari nimewajenga uwezo na umakini kwenye mazoezi” alisema Kondo.
Aidha, Villa jana mchana ilitarajia kuingia bungeni kufuatia mwaliko wa Mbunge wa Kinondoni ambaye pia ni mdau wa timu hiyo, Idd Azan.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment