Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassin Ng’amilo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana juu ya utekelezaji wa mradi uwekaji boya jipya la mafuta.
*******************************************************
TAARIFA KUHUSU UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI NA UWEKAJI WA BOYA JIPYA LA MAFUTA (SINGLE POINT MOORING – SPM)
UTANGULIZI
Mradi wa ujenzi uwekaji wa boya jipya la kupakulia mafuta yaliyosafishwa (white products) na yasiyosafishwa (crude oil), ulitiwa saini kati ya Mkandarasi “M/s. Leighton Offshore Pte mwenye makao makuu Singapore na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) tarehe 30 Septemba 2010. Mradi huu ambao unategemewa kukamilika mwezi April 2012 utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 70 (sabini) kwa pesa za TPA na mkopo kutoka Benki ya CRDB.
Mradi utakapomalizika utaongeza uwezo wa upakuzi wa mafuta kutoka meli za ujazo wa 40,000 kufikia meli zenye ujazo wa tani 150,000 (Laki moja na hamsini) katika kina cha maji chenye urefu wa mita 25. Boya linalowekwa litakuwa na mabomba mawili, moja la inchi 28 kwa ajili ya mafuta meusi (crude oil) na la pili inchi 24 kwa ajili ya upakuaji wa mafuta yaliyosafishwa (petrol, diesel, kerosene, JetA1) ambayo yatatambaa kupitia chini ya Bahari kwa takribani km 3.6 na km 4.3 chini ya ardhi hadi Kigamboni ambapo bomba la mafuta meusi litaelekezwa TAZAMA na la mafuta yaliyosafishwa litaendelezwa mpaka kwenye matanki ya kuifadhi mafuta kwa muda (custody transfer tanks) itakayojengwa Kurasini karibu na Dock yard.
HALI HALISI YA MRADI
Mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi huko Kigamboni mnamo April 2011. Kazi ya kutandaza mabomba katika nchi kavu ilianza mwezi August 2011 na mpaka sasa kazi hiyo imefikia zaidi ya asilimia 60. Kazi ya kutandika bomba majini ilianza December 2011, na meli (barge) ya kutandika mabomba hayo (Stealth Leighton) imeishafika hapa bandarini na inatarajiwa kuelekea kwenye boya kesho ijumaa ya tarehe 27/01/2012.
Kazi hii yote ya kuweka boya, kulaza mabomba ndani na nje ya bahari, na kuunganisha bomba la mafuta meusi kwenye matangi ya TAZAMA na mafuta yaliyosafishwa KOJ imepangwa kumalizika mwezi Aprili 2012. Majaribio ya mradi huu (pre-commissioning) yanategemea kuchukua muda wa miezi miwili. Kazi ya kuudumia meli za mafuta itaanza rasmi mwezi Julai 2012.
FAIDA ZA MRADI HUU
1. Meli zitakuwa zinapakuliwa kwa muda mfupi. Kwa mfano, mafuta yasiyosafishwa (crude oil) yatapakuliwa kwa mita za ujazo wa 3,500 kwa saa, na mafuta yaliosafishwa yatapakuliwa kwa mita za ujazo wa 2,500 kwa saa. Meli yenye tani 150,000 ya mafuta yaliyosafishwa itapakuliwa SPM kwa muda wa masaa 75 (siku tatu), ukilinganisha na KOJ ambapo meli yenye ujazo wa Tani 40,000 unachukua siku 4 mpaka 5 ya kupakua.
2. Kupunguza msongamano wa meli kusubiri kupakua mafuta katika Gati ya mafuta ya Kurasini (KOJ).
3. Ujenzi wa mradi huu wa SPM utawezesha uagizaji wa mafuta kwa meli kubwa zaidi kuliko ilivyo sasa na utasaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa mafuta.
Imetolewa na
Cassin Ng’amilo
MENEJA WA BANDARI YA DAR ES SALAAM
meli ndogo ambayo inatumika kuvuta boya la mitambo.
Hii ni moya ya vifaa vya mawasiliano vilivyopo Control room.
Meli hiyo kubwa ina uwanja wa Helicopter juu.
Hili ndo dude lenyewe la mitambo ya kutandazia mabomba baharini
Control room ndio hiii na hapa kila kitu kinaongopzwa
wabnahabari walipokuwa wakiingia katika Karakana hiyo.
Wakisikiliza maelezo
mabomba yakishaungwanishwa humo ndani kabla ya kuteremshwa baharini lazima waangalie iwapo hayavuji na yameunganishwa vyema, hivyo huu ndio mtambo wa X Ray, wanadai unamionzi mikali sana mna yahatari.
Mtaalam wa ujenzi huo akifafanua jambo, kulia ni Ofisa Uhusiano wa bandari Peter Milanzi
Mafundi watakao fanya kazi hiyo. wapo zaidi ya 100.
wanahabari wakiwa katika chumba cha Mikutano ndani ya Karakana hiyo.
Moja ya mabomba yatakayo kuwa yakiwekwa
0 comments:
Post a Comment