Msanii Mkongwe katika tasnia ya Maigizo/Filamu hapa nchini,Fundi Saidi almaarufu kwa jina la kisanii Mzee Kipara amefariki mapema leo asubuhi,nyumbani kwake huko Kigogo Mbuyuni-Kinondoni jijini dar.
Mzee kipara ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1922,huko Bongoni mkoani Tabora,alikuwa kisumbuliwa na matatizo ya miguu kukosa nguvu,alikuwa hawezi kusimama mwenyewe,sambamba na umri nao huenda ulichangia kwa maradhi hayo na mengineyo,hali iliyokuwa ikimlazimu kutumia muda mwingi kitandani,wakati mwingine alishindwa kutoka nje mpaka watu watokee kumtoa nje ili kuota jua ama kupunga upepo.
Mzeee Kipara alianza sanaa mnamo mwaka 1964 kwa kufanya kazi za mitaani na baadaye akachukuliwa na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) sasa TBC Taifa. Akiwa na kituo hicho, aliigiza katika michezo mingi na nafasi zake kubwa zilikuwa zile zenye kuonesha utemi, wengi huita ukorofi. Mnamo Mwaka 1999, akiwa na wasanii wenzake akina Zena Dilip, Rasia Makuka, marehemu Rajab Hatia ‘Mzee Pwagu’ na Mama Haambiliki walijiunga katika Kundi la Kaole ambalo lilikuwa likirusha maigizo yake katika Runinga ya ITV.
Taarifa zaidi za msiba huo na mazishi tutafahamishana zaidi hapo baadaye kidogo.MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI -AMIN.
0 comments:
Post a Comment