Mpendwa msomaji wa Blogu hii kuanzia kila ijumaa nitakuwa nakuletea mambo machache muhimu ya kijamii ambayo huzungumzwa na abiria NDANI YA DALADALA kila siku.
Hivi juzi nilikuwa katika daladala linalofanya safari zake kati ya Posta na Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. Nilikuwa miongoni mwa abiria kibwena tuliosheheni katika daladala hilo aina ya DCM “Ndoki” nadhani ni mali ya tajiri JJ Karan lile.
Garini humu mimi nilikuwa kiti cha pili kutoka nyuma, kando yangu walikuwa wameketi akina mama watatu, kwa mujibu wa mazungumzo yao ya hapa na pale juu ya maisha ya kila siku katika maeneo wanayoishi pamoja na kuzungumzia masuala ya kazi zao nikaja kubaini kuwa hawa wote kazi wanayo fanya ni moja ila tu wanatoka vituo tofauti vya kazi.
Ndio, wamama wale wa makamo walikuwa ni Walimu wa shule zetu za Vijiji. Hahaha ndio Shule ya Kijiji nikimaanisha shule ya Msingi, kwani wewe wa wapi hadi hujui kama Sekondari ndio Shule ya Kata tena ile ya serikali.
Basi walimu wale wa Jamii na Familia walizungumza mengi kuhusiana na kazi yao na kila mmoja anavyo weza kumudu kufanya kazi yake bila wasi huku darasani akiwa na halaiki ya watoto walioketi chini mithili ya mkutano wa hadhara kijijini kwetu Kipera.
Walipomaliza kujadili ya kazi zao sasa wakahamia katika mada ya malezi ya familia. Hapa japo nilikuwa nikisinzia kutokana na joto kali lililopo ndani ya DCM lile pamoja na foleni nikawa nasikiliza kwa mbali mada yao.
Mazungumzo yao yaliendelea na kubwa zaidi wakazama katika malezi ya watoto wao, na hasa si wao wanao leo bali vile wadada wa kazi nyumbani wanavyolea watoto. Mmoja alidai kuwa yeye mdada wake anapenda sana mtoto muda mwingi yupo nae, mwingine akasema yeye msichana wake ni jeuri lakini hana jinsi anaendfelea tu kuishi nae kwakuwa hajapata mwingine na anafikiria hata kutafuta mvulana.
Yes wasichana siku hizi ni adimu sana siunajua Shule za Kata na siku hizi ukimpata msichana kutoka kijijini basi ujue kama hajaishia kidato cha pili basi kamaliza kidato cha nne.
Basi bwana! Mwalimu mwingine yeye akasema yale mabayo binti yake aliyemfukuza alikuwa akimfanyia mtoto wake wa kiume, mh! Alilosema lilinishtua katika kausingizi kale na klumuangalia yule Mwalimu.
Alidai kuwa binti huyo siku moja aliporudi mchana ghafla akitoka kazini alimkuta yupo na mtoto katika korido uchi kama walivyo zaliwa. Mama alishtuka sana kuona vile na kumuuliza nini alikuwa akifanya ni mambo ya kichawi au nini lakini kabla hajapata jibu lolote alikasirika sana na kumuamuru afungashe kila kilicho chake aondoke zake.
Anadai aliona kitendo cha kusikiliza maelezo ya nini alikuwa anafanya kingemuumiza zaidi na zaidi aliamua kumtimua. Pale pale mwingine akadakia kuwa jirani yake alibaini kuwa mtoto wao wa kiume darasa la tano alikuwa akibakwa na binti wa kazi mara kwamara lakini mbaya mtoto yule nae alikuwa amesha zoea. Anasema walibaini katoto kanamaaka asubuhi kamechoka sana siku moja walimkuta anakachezea sehemu zake maridhawa nako kakimshika shika binti wa kazi huko kunako jinsia yake.
Lakini mbali na kusikia katika daladala mimi niliwahi kusikia kutoka kwa swahiba wangu kuwa beki tatu wake alikuwa akifanyisha mapenzi kijana wake mdogo. Sasa jamii yetu hakika inapokwenda tunaenda wapi… na unaweza jiuliza wapi ni wema kuweka mvulana, au msichana wa kazi?
Wakadai yote ni balaa ila mmoja akasema yaani kuliko huyo binti kucheza na watoto wake ni heri acheze mchezo huo na Mumewe! Nikashtuka na kulazimika kuingilia maongezi ya Walimu wangu wale kusema yaani utamruhusu beki tatu ahudumiwe na Mzee?
Mh nikaona huyu mama kafika mbali sasa nikasema kwani kuliko kufanya hivyo ni bora umruhusu tu kila mwisho wa wiki aende kutembea kasha jioni arudi hapo akili itamkaa na kutambua ruhusa ile ni yanini.
Dah! Wao walifika mwisho wa safari yao na mimi na abiria wengine tuliendea na safari hadi Posta mpya safari ilifikia tamati.
Ndugu zangu hili likanifundisha kuwa wazazi hatuna budi kuwa karibu sana na watoto wetu wa kiume pale nyumbani ili kubaini kama kuna lolote linaendelea kati yao na hao tunaow3aita dada zao. Maana kutokufanya hivyo ni kuharibu familia
Hiyo ni NDANI YA DALADALA......!!!!
Hadi siku ingine….!!
Ukiwa na maoni au ushauri au kisa ulichosikia katika daladala
Kitume mrokim@gmail.com 0717002303
jee visa vya dalaa dala tu au vyombo vyovyote vya usafiri wa abiria,vile vile unataka vya Tanzania tu au njee pia ya Tanzania,,, Aidha kama njee ya tz unavitaka mimi nipo unyamwezini jeee unavitaka visa vya unyamwezini faza...? maana vipo mpaka kwenye matraini tupe jawabu uanze kazi au la Abou Muze wa swahilivilla
ReplyDeleteEbou's wewe tuma tu hakuna noma tena ndo itakuwa nzuri maana tutapata kuona wazungu wanapiga soga zipi katika daladala zao ambazo ndo ndo hizo treni nk. RUKSA
ReplyDelete