"Naipenda sana Kilombero. MUNGU nisaidie nitimize ndoto zangu za kuwatumikia vyema Wananchi wanaoniamini na kunitegemea.Amen"
Haya si maneno yangu bali ni maneno yake mwenyewe Marehemu Rejia Mtema aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Kilombero Mkoani Moprogoro. Hakika Kifo hakina huruma na laiti kama yeyote kati yetu tulio hai bado twavuta pumzi ya Mwenyezi Mungu basi tusinge kikariba hata kwa nini... Hivi unadhani leo Rejia angejua kuwa kifo chake kitachukuliwa na gari yake mwenyewe unadhani angeiendesha leo... Lahasha lakini siri hii ndioinatufanya tuendelee kuachana na wapendwa wetu bila hata kutuaga.
Lakini maneno haya ya Marehemu ambayo mwwenye aliyatamka na kuyaweka kimaandishi katika ukurasa wake wa marafiki wa Facebook ndio yamenitia simanzi kubwa mimi na hasa kama mkazi wa Morogoro. Kweli Rejia aliwapenda sana wakazi wa Kilombero na pia naimani nanyi mlimpenda sana lakini Mungu katuzidi katika hayo mapenzi.
Pumzika Rejia
Wengi tutakulila,
Ulionesha yako nia,
Maendeleo kupigania.
Ajali haina kinga,
Katu hilo sitopinga,
kwa kisu hata mizinga,
Tangulia dada Rejia.
Mimi nina kulilia,
Wapo wengi wanalia,
Si Chadema na CCM Pia,
Yupo Mbowe hapa analia.
Ulikuwa bado kijana
Tena ungali msichana,
Mauti yamekufika mchana,
Tangulia dada Rejia Mtema.
Wamoro kwetu ni pigo,
Wanakulilia Makala, Nkya na Abood,
Nani ataziba lako Pengo,
Ulale pema Rejia.
Mauti yamemfika akiwa njiani kuelekea Mkoani Morogoro ambako bila shaka ni katika eneo lake la Kilombero kuwatumikia wana Kilombero na huko lazima kuna misaada au shughuli mbalimbali za maendeleo alikuwa akizipeleka.
Huu hapa chini ni wasifu wa Marehemu Rejia Mtema kama ulivyo katika tovuti ya Bunge la Tanzania.
EDUCATIONS | ||||
Start Date | End Date | Level | ||
Sokoine University of Agriculture, SUA | BSc. (Home Economics & Nutrition) | 2003 | 2006 | GRADUATE |
Machane Girls Secondary School | A-Level Education | 2000 | 2002 | HIGH SCHOOL |
Forodhani Secondary School | O-Level Education | 1996 | 1999 | SECONDARY |
Mchikichini Primary School | Primary School Education | 1989 | 1995 | PRIMARY |
CERTIFICATIONS | ||||||
Certification Name or Type | Certification No. | Issued | Expires | |||
No items on list | ||||||
EMPLOYMENT HISTORY | |||
Company Name | Position | From Date | To Date |
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA | Principal Training Officer | 2007 | 2010 |
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA | Principal Youth Officer | 2007 | 2009 |
Chama Cha Malezi na Malezi Bora (UMATI) | Internship | 2006 |
POLITICAL EXPERIENCE | |||
Ministry/Political Party/Location | Position | From | To |
CHADEMA | Member - General Committee | 2009 | |
CHADEMA | Youth Training Officer | 2007 | |
CHADEMA | Member | 2005 | Todate |
PUBLICATIONS | ||||||
Description | Published Date | |||||
No items on list | ||||||
SPECIAL SKILLS | ||||||
Years Experience | Acquired Through | Skill Level | ||||
No items on list | ||||||
MAY THE ALMIGHTY GOD REST HIS SOUL INTO PEACE AMEN.MAY THE GOD`S WORD CONSOLE HER PARENTS,FAMILY FRIENDS AND THE NATION OF TZ.AS A WHOLE.
ReplyDelete