Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu , Peniel Lyimo akiwa ameshikilia ripoti ya Maendeleo Duniani 2011 Human Development mara baada ya kuizindua jijini Dar es Salaam Novemba 3, 2011. Kulia ni Resident Coordinator and UNDP Resident Representative Alberic Kacou.
*************************
Mwelekeo wa Mazingira watishia maendeleo ya maskini ulimwenguni, yaonya Ripoti ya Maendeleo ya Dunia ya Mwaka 2011
*Masuala ya afya, kukua kwa kipato katika nchi zinazoendelea yatishiwa na ukosefu wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, uharibifu wa mazingira, Ripoti inaonyesha
*Tofauti za ukwasi na jinsia zahusishwa na athari za mazingira
Copenhagen, Novemba 2, 2011—Kasi ya maendeleo katika nchi zinazoendelea yaweza kusimama au hata kurudi nyuma ifikapo katikati ya karne hii, iwapo hatua thabiti hazitachukuliwa hivi sasa kupunguza kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa, kuzuia uharibifu wa mazingira, na kupunguza ukosefu mkubwa wa usawa wa maendeleo ndani ya mataifa, kulingana na Ripoti ya Maendeleo ya Dunia ya Mwaka 2011, ambayo
ilizinduliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa hivi leo.
Ripoti ya 2011—Uendelevu na Usawa: Mustakabali Bora Kwa Wote Inatoa hoja kwamba uendelevu wa mazingira waweza kufikiwa kwa njia ya haki na yenye matokeo mema iwapo masuala ya afya, elimu, kipato, na tofauti za jinsia pamwe na kuchukuliwa hatua za kimataifa kuhusu uzalishaji wa nishati na utunzaji wa mazingira yatashughulikiwa.
Wakati jumuiya ya kimataifa inajiandaa kwa kikao muhimu cha Umoja wa Mataifa cha Maendeleo Endelevu mnamo mwezi Juni, 2012 huko Rio De Janeiro, Ripoti inawasilisha hoja kwamba suala la uendelevu lichukuliwe kama jambo la haki ya msingi ya jamii, kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.
“Uendelevu si suala ambalo awali ya yote linahusiana na mazingira, au ni la mazingira kwa namna zote, kama Ripoti hii ya kuvutia inavyosema,” Helen Clark anasema katika utangulizi. “Kimsingi, uendelevu unahusu jinsi ambavyo tunachagua kuendesha maisha yetu, tukitambua kwamba kila tutendalo lina athari kwetu sisi watu bilioni saba tuliopo hivi leo, pamoja na mabilioni ambao watafuata karne nyingi zijazo.”
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa limeanzisha Ripoti ya Maendeleo ya Dunia, ambayo uhuru wake hauingiliwi, tangu mwaka 1990, ambapo Farihisi ya Maendeleo ya Dunia, ambayo ni kipimo mshirika cha afya, elimu, ilipotoa changamoto kwa mara ya kwanza kuhusiana na tabia ya kupima kiwango cha maendeleo kwa kuzingatia takwimu za uchumi tu katika kupima maendeleo ya taifa na ikatoa wito wa kuwepo kwa shughuli mfulizo za kufuatilia upigaji wa hatua katika maeneo yote ya viwango vya maisha.
Kati ya mwaka 1970 na 2010, nchi zilizokuwa kwenye kundi la asilimia 25 ya chini kabisa kimaendeleo kufuatana na tathmini ya Farihisi ya Maendeleo ya Dunia ziliboresha utendaji wao kwa asilimia ya kuvutia ya 82%, ambayo ni mara mbili ya wastani wa dunia. Iwapo kasi ya kupiga hatua iliyoonekana katika kipindi cha miaka 40 iliyopita itaendelea kwa miaka 40 mingine, idadi kubwa kabisa ya nchi itafikia viwango vya Farihisi ya Maendeleo ya Dunia ifikapo mwaka 2050, ambavyo vitakuwa sawa au zaidi ya vile vya nchi zilizo katika fungu la asilimia 25 ya juu kabisa kwa makadirio ya hivi sasa, Ripoti inaainisha—jambo hili litakuwa mafanikio yasiyokuwa ya kawaida ya dunia ndani ya kipindi kisichofikia nusu karne.
Hata hivyo, kutokana na kukua kwa uharibifu wa mazingira, maendeleo haya mazuri yaweza kukwamishwa ghafla kabla ya nusu karne, Ripoti inasema., ikizingatia kwamba watu katika nchi maskini kabisa wako katika hatari inayozidi kiwango inayotokana na majanga yanayohusiana na hali ya hewa kama ukame na mafuriko, na kuwepo kwa watu katika maeneo yenye uchafuzi wa hewa na maji.
Uendelevu na Haki ya Jamii Licha ya maendeleo yaliyofikiwa katika miaka ya karibuni, ugawaji wa kipato umezidi kuwa mbaya, kuna tofauti za kutisha za jinsia ambazo bado zipo, na kasi inayoongezeka ya uharibifu wa mazingira inazitwisha “zigo la ufuke lenye uzito mara mbili” kaya na jumuiya ambazo ni maskini kabisa, Ripoti inasema.
Hali ya maisha ya hali ya juu haitakiwi ichochewe na kuwepo kwa carbon kwa kufuata mfano wa nchi tajiri kabisa ulimwenguni, Ripoti inasema, ikitoa ushahidi kwamba utokezi wa hewa ya carbon dioxide umeoanishwa kwa karibu na kukua kwa pato la taifa katika miongo ya hivi karibuni, ambapo matumizi ya nishati inayotokana na masalia ya kale ya wanyama na mimea hayaendi sambamba na vigezo vingine vya maendeleo ya mwanadamu, kama wastani wa umri wa kuishi na elimu. Kwa hakika, nchi nyingi zilizoendelea zinapunguza kiwango cha hewa chafu inayozalishwa wakati huohuo zikidumisha kasi yao ya kukuza uchumi.
“Ukuaji wa uchumi unaosukumwa na matumizi ya mafuta yatokanayo na masalia ya kale ya wanyama na mimea si sharti linalotangulia kutimizwa ili kupata maendeleo ya mwanaamu yenye maana pana zaidi,” Helen Clark anasema. “Uwekezaji ambao unaboresha, mathalani, upatikanaji wa nishati jadidika, maji na huduma za kuondoa uchafu, pia huduma za afya ya uzazi—vyaweza kuboresha uendelevu pamwe na maendeleo ya mwanadamu.”
Ripoti inatoa wito wa kupelekewa umeme watu bilioni 1.5 ulimwenguni ambao wako nje ya mfumo wa usambazaji wa umeme—tena inatamka kuwa hatua hii inaweza kutekelezwa katika hali ambayo wanunuzi watapata nishati endelevu kwa bei iliyo ndani ya uwezo wao, bila kuwepo kwa ongezeko kubwa la uchafuzi wa hewa.
Hii “Juhudi Mpya ya Kupata Nishati Duniani” ambayo inaungwa mkono na Umoja wa Mataifa, yaweza kufanikishwa na uwekezaji wa takriban moja ya nane ya kiasi ambacho kinatumika kwa nishati mbadala wa masalia ya kale ya wanyama na mimea inayokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 312 katika dunia nzima mnamo mwaka 2009, kufuatana na Ripoti.
Ripoti inaongeza sauti ya wale wanaohimiza kufikiriwa kwa kodi ya kimataifa ya biashara au aina pana zaidi ya ushuru wa dharura ya biashara ili kupata fungu la kugharamia mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa na umaskini uliokithiri.
Ushuru wa aslimia 0.005 wa dharura ya biashara ya nje ungeweza kukusanya dola bilioni 40 au zaidi kwa mwaka, Ripoti inakadiria, hatua ambayo itaongeza kwa kiasi kikubwa mtiririko wa misaada kwa nchi maskini—iliyofikia dola za Marekani bilioni 130 mnamo mwaka 2010—kwenye kipindi ambacho upatikanaji wa fedha za misaada zilizoahidiwa unapungua kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani.
“Kodi hii ingewawezesha wale wanaonufaika zaidi na utandawazi kuwasaidia wale ambao hawajanufaika sana,” Ripoti inadai, ikikadiria kwamba takriban dola za Marekani bilioni 105 zinahitajiwa kwa mwaka ili kugharamia namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, hususan katika Asia Kusini na nchi za Afrika Zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Ripoti inainisha mambo ya kijamii ambayo mara nyingi hayahusishwi na uendelezaji wa mazingira:
Kuongezeka kwa haki za uzazi, huduma za afya na kinga ya uzazi kungefungua ukurasa mpya katika mapambano dhidi ya tofauti za jinsia na umaskini, Ripoti inajiridhisha. Haki za uzazi zaweza kupunguza uzito wa matatizo ya mazingira kwa kupunguza ukuaji wa idadi ya watu duniani, ambayo inakadiriwa itaongezeka toka idadi ya watu bilioni 7 hivi leo hadi bilioni 9.4 ndani ya miaka 40 ijayo.
• Ripoti inadai kuwa vyombo huru na rasmi vya kufuatilia utendaji—ambavyo ni pamoja na vyombo vya habari, makundi ya kiraia na mahakama—vina umuhimu
kwa ushiriki wa raia katika uundaji wa sera ya mazingira. Katiba za mataifa
120 zinahakikisha utunzaji wa mazingira, hata hivyo kuna utekelezaji hafifu wa
vifungu hivyo vya katiba katika nchi nyingi, Ripoti inasema.
• Hatua thabiti za kimataifa zahitajiwa kuchukuliwa ili maendeleo endelevu
yapatikane, na juhudi mahalia za kusaidia jumuiya maskini zaweza kufanikiwa
kwa kutumia gharama ndogo na kuwa za manufaa kwa mazingira, Ripoti
inasisitiza. Nchini India, utekelezaji wa Sheria ya Kuhakikisha Kuwepo kwa Ajira
Vijijini uligharimu kama asilimia 0.5 ya pato la taifa na kunufaisha kaya milioni
45, ikiwa sawa na moja ya kumi ya watu wote walioajiriwa nchini India.
•
Miradi ya Bolsa Familia wa Brazil na Oportunidades wa Mexico iligharimu asilimia
0.4 ya Pato la Taifa na kuweka mipangilio ya kuzuia majanga kwa moja ya tano ya
wananchi.
Waandishi wa Ripoti walitabiri kwamba kutothibiti uharibifu wa mazingira, kuanzia
ukame katika nchi za Afrika Zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara na kupanda kwa usawa
wa bahari ambao waweza kuzifunika nchi zilizo maeneo ya chini kama Bangladesh—na
kusababisha kupanda kwa bei ya vyakula hadi asilimia 50 na kurudisha nyuma juhudi za
kuongeza upatikanaji wa maji, huduma za kuondoa uchafu na nishati kwa mabilioni ya
watu, hususan wale wa Asia Kusini na nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Sahara.
Ifikapo mwaka 2050, katika taswira ya “changamoto za kimazingira” itakayoonekana
kwenye matokeo ya uzalishaji wa chakula na uchafuzi wa mazingira, wastani wa Farihisi
ya Maendeleo ya Dunia utakuwa chini kwa asilimia 12 katika Asia Kusini na nchi za
Afrika Zilizo Kusini wa Jangwa la Sahara kuliko iwapo hali ingekuwa tofauti, Ripoti
inakadiria.
Kwenye taswira mbaya zaidi ya “janga la kimazingira”—yenye ufyekaji holela wa
misitu, kupungua sana kwa viumbehai na kuongezeka kwa hali mbaya ya hewa, Farihisi
ya Maendeleo ya Dunia kwa mataifa yote itashuka kwa asilimia 15 chini ya makadirio ya
mwaka 2050, hasara kubwa zaidi ikiathiri nchi zilizo maskini kabisa.
Kuharibika kwa mazingira kwaweza kuziharibu juhudi za kuongeza upatikanaji wa
huduma za maji, uondoaji taka, na umeme kwa jamii maskini kabisa duniani. “Ukosefu
kamili wa huduma hizi, ambazo ni muhimu kabisa, ni uvunjaji mkubwa wa haki za
binadamu,” waandishi wanasema.
KUHUSU RIPOTI HII: Ripoti ya Maendeleo ya Dunia itolewayo kila
mwaka ni chapisho huru la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP). Ukitaka kupata Ripoti ya Maendeleo ya Dunia bila malipo, pamoja
na makala za ziada za marejeo ya farihisi zake au kishindo chake katika
maeneo mbalimbali, tafadhali tembelea: http://ddr.undp.org.
KUHUSU SHIRIKA LA MAENDELEO LA UMOJA WA MATAIFA
(UNDP): Shirika hili linashirikiana na watu wote katika ngazi zote za jamii
katika kujenga mataifa yatakayoweza kukabili migogoro, kusukuma na
kudumisha aina ya maendeleo yatakayoboresha maisha ya kila mtu. Likiwa
na ofisi katika nchi 177 ulimwenguni, Shirika linatoa taswira ya dunia na
kuleta mwanga wa ufahamu ndani ya nchi husika ili kuwezesha maisha ya
watu na kujenga mataifa thabiti. Tafadhali tembelea: www.undp.org.
0 comments:
Post a Comment