Nafasi Ya Matangazo

November 23, 2011

Ofisa mawasiliano wa Airtel Dangion Kaniki ( kushoto) akikabidhi Tshirt kwa mwenyekiti wa tamasha la wiki ya Vitabu bwana Abdallah Hassan ikiwa ni moja kati ya mchango wao katika kudhamini wiki ya vitabu itakayoanza kesho tarehe 23 hadi 26 mwenzi katika maktaba ya taifa.

Kampuni ya simu Airtel Tanzania kwa kushirikia na Taasisi ya maendeleo ya vitabu ya taifa  imefanikisha maonyesho ya 20 ya vitabu taifa kufanyika mwaka huu ambapo uzinduzi wake utafanyika rasmi kesho tarehe 23 /11/2011katika maktaba ya taifa jijini Dar-es- salaam kuanzia tarehe 23/11/2011 hadi tarehe 26/11/2011 .

 Akiongea kwa niaba ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel meneja mahusiano wa Airtel bw Jackson Mmbando amesema "Airtel inajisikia furaha kudhamini wiki hii ya kusoma vitabu yenye lengo la kujenga tabia ya kusoma vitabu  kwa jamii nzima kwani tunaamini ni njia kubwa ya kuongeza ufahamu na elimu katika jamii na nchi kwa ujumla. udhamini huo ni muendelezo wa program ya Kampuni yetu katika kufanikisha maendeleo ya sekta ya elimu nchi".
 
Tunaamini  usomaji wa vitabu mbalimbali ni njia mbadala ya kujikomboa na ujinga na umaskini ambao umekuwa ni tatizo kubwa kwa watanzania kwani tunajipatia taaluma yakutosha, aliongeza Mmbando

Kwa upande mwingine mwenyekiti wa tamasha la wiki ya vitabu Bw.Abdallah Hassan ameishukuru Airtel Tanzania kwa kudhamini tamasha hilo kwa mwaka huu na kuwaomba waendelee kushirikiana nao katika programme mbalimbali zilizoko mbeleni.
 
Aliongeza kwa kusema "Maonyesho haya ya vitabu yataudhuriwa na waandishi kutoka nchi za  jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi nyingine za kigeni pia wauzaji wa vitabu ,wachapishaji wa vitabu,maktaba mbalimbali,taasisi za elimu za kitafiti,Asasi za kiraia,balozi mbalimbali na mashirika mbalimbali.

Hii ni fulsa pekee kwa watanzania kutembelea katika viwanja vya maktaba yetu na kujionea na kujipatia vitabu mbalimbali. Aidha tunawaamasisha wazazi na walezi kuwaleta watoto wao katika maonyesho hayo na kushiriki katika programme nyingi zilizoandaliwa zenye lengo la kuhamasisha usomaji wa vitabu katika umri  mdogo.
Posted by MROKI On Wednesday, November 23, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo