Licha ya kuwa nchi yetu inaadhimisha miaka 50 ya Uhuru lakini bado baadhi ya wananchi wamekuwa wakinyanyasika na hao waliokuwa wakoloni wa nchi ya Tanganyika. Pichani ni mzaliwa wa Kinyenze, Mroki Mroki akipita katika uzio wa mwekezaji Mzungu aliyefunga njia kwa mabavu na kuzuia wananchi wengine kwenda majumbani kwao na mashambani.
Ni baiskeli tu tena hizi ndogo yawezakupita hapo au kuivusha kwa kuibeba. Pichani ni Nuru James akipita kwa tabu na baiskeli yake na kulalamika kuwa njia hiyo ni ya kupitishia mifugo na si binadamu, maana imewekewa uzio mwembamba ulio kama V. Mbunge waJimbo la Mvomero Amos Makalla hivi karibuni alifika na kujionea njia hiyo iliyofunguliwa na kuahidi kuendelea kufuatilia suala hilo na barabara ya kupitisha magari ifunguliwe bila masharti na watu waendelee kulima mashamba yao.
Mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera Kata na Tarafa ya Mlali, Bi. Mary Nathan akipita katika njia ndogo iliyofunguliwa na Mwekezaji huyo baadaya wananchi wa kijiji hicho kulalamika kufungwa kwa njia hiyo kuu iendayo katika mtaa wa Mwanga na mashambani. Pia mwekezaji huyo amechukua mashamba kadhaa ya wananchi hao. Licha ya kufunguliwa kwa njia hiyo na Mzungu lakini mbali na baiskeli hakuna usafiri wa aina nyingine unaoruhusiwa au kuwezakupita katika eneo hilo jambo ambalo badoo limekuw ni kero kwa wananchi na kujiona watumwa katika nchi na ardhi yao.
Ama kweli halafu bado serikali inakaa kimya hakuna anayesema chochote! Tatizo ni kuwachagua hawa viongozi wasiojali maslahi ya wananchi; wao wanajali matumbo yao tu. Haiwezekani wananchi wakafungiwa njia na mtu mmoja tena basi mwamiaji. watu wanashindwa kufanya shughuli zao; maisha yenyewe tayari ni magumu. Inasikitisha sana...
ReplyDelete