Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi ya Viongozi, kubeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja leo Agosti 24.Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif na baadhi ya viongozi wakiwa katika dua ya kumuombea aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Unguja, marehemu Mussa Hamis Silima, aliyefariki Agosti 23 katika hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam, alikolazwa baada ya kupata ajali Agosti 22. Marehemu Silima amezikwa leo Agosti 24 katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja.Rais wa Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakiwa katika shughuli ya mazikonya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Silima.
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima.
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima.
Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Mambo ya nje ya Bunge Edward Lowasa akiweka odongo.
Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe akiweka udongo.
Wakazi wa Kijiji cha Kiboje na vitongoji vyake wakijumuika katika shughuli ya maziko ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja leo.
0 comments:
Post a Comment