Nafasi Ya Matangazo

August 09, 2011

Salaam kwako ndugu yangu.
Natumai kuwa u-mzima na unaendelea vema na harakati za mapambano ya maisha.. Nami pia.

Sababu pekee ya wewe kupokea UJUMBE HUU BINAFSI siku hii ya leo ni kwa kuwa umekuwa sehemu ya maisha yangu ndani miezi 12 iliyopita ama zaidi. Hivyo ninaposherehekea siku yangu ya kuzaliwa (Aug 10), napenda kuleta ujumbe huu mfupi wa SHUKRANI ZANGU ZA DHATI kwa namna ulivyoendelea kuwa mmoja wa wale wanaoyafanya maisha yangu kuwa yalivyo sasa. 
Iwe ni kwa MANENO, MATENDO ama MAWAZO yako.
Nathamini sana uwepo wako na nakuombea mafanikio katika kila lililo jema utendalo ila maisha yako yawe mfano mwema kwa wengine wengi.

Nikumbushe tu kwamba, katika maisha yetu na katika kila jambo tutendalo, "kuna anayetuona kwa mara ya kwanza na / ama mara ya mwisho" na swali ni kuwa TUNAMUACHA NA TASWIRA GANI KUHUSU SISI NA MAISHA YETU?
Unapendwa, Unakumbukwa na UNAOMBEWA MEMA ASANTE KWA KUWA ULIVYO


http://www.changamotoyetu.blogspot.com
http://www.youtube.com/user/mutwiba
Posted by MROKI On Tuesday, August 09, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo