Nafasi Ya Matangazo

March 23, 2011

Maadili yanapo potoshwa...
Kizazi kinapokosa heshima na adabu katika jamiia
Hivi ndivyo kizazi cha wasichana wa siku hizi wanavyo vaa na kuweka mambo yao ya falagha hadharani, zamani ilikuwa ni nandra kumuona mwananke akiwa amevaa shanga "chachandu" nje namna hii. Na vitu hivi hupaswa kuvaliwa kwa heshima. Je hii ndo kwenda na fasheni au tunawafundisha nini watoto wetu? . Picha hii imepigwa jijini Dar es Salaam katika daladala msichana huyu akiteremka kituoni.
Posted by MROKI On Wednesday, March 23, 2011 6 comments

6 comments:

  1. ukosefu wa adabu,uchafu na kujidharau mwenyewe!!!!!
    baadhi ya wanawake/wasichana wa siku hizi hawajiheshimu na kujithamini kabisa, inatia kinyaa! si kila kiingiacho ni kuiga tuu.

    samahani nimewaza kwasauti!!!.

    ReplyDelete
  2. Duuh hito kali yaani ni aibu ya mwaka! Hivi vitu havitakiwi kuonwa kabisa hadharani. Lakini sasa na hiyo fasheno ya surua;i kuacha makalio na vingine nje haipendezi kabisa.Wanawake kama kwenda na wakati huko siko kabisa..kwani ni aibu tupu.

    ReplyDelete
  3. Kaka kwa chabo tu, nakuaminia

    ReplyDelete
  4. Ni kweli si kitu cha kuvaliwa hadharani kila mtu akuone. Binti huyu anatuaibisha wanawake na pia naona kwa umri wake ni mapema mno kufanya mambo hayo.tujifunze jamani kuna wakati maalum wa kuvaa chachandu si muda wote.

    ReplyDelete
  5. Ndiyo utandawazi huo kaka usishangae sana.

    Pengine tujiulize, hayo maadili tunayoyalilia kuyadumisha ni yapi? Yangalipo? Ni nani anayepaswa kuyadumisha, kuyatetea na kuyalinda?

    Unafikiri kwenye jamii ambayo wachache ndiyo wanamiliki kila kitu, jamii ambayo imepoteza mwelekeo kiasi kwamba mafisadi na wezi ndiyo wanaonekana kama mashujaa, kuna maadili tena?

    Tusichukue punje moja moja bali tuliangalie kapu zima la mchele. Hali si nzuri katika jamii na pengine kumlaumu binti huyu si haki. Tatizo ni kubwa zaidi kuliko inavyoonekana!

    ReplyDelete
  6. Brother

    Mwenzenu mimi Demu awe na chachandu asiwe nazo me wala sioni tofauti yoyote!

    We Mroki vipi huwa unazimissigi hizo?

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo