Mkazi wa Kichangani ndani ya Manispaa ya mji Kasoro Bahari Morogoro, Fatma Senga ambaye nae amefuata nyayo za babu wa Loliondo, Kaka wa Mbeya , Dada wa Tabora na hivi sasa ni yeye Mama wa Kichangani Morogoro anayetoa dozi ya kipimo cha kikombe/Glasi.
Huyu yeye hana kipimo maalum na vikombe vyake kwa jinsi vilivyoonekana ni vile vidogo vya Chai na Bilauri za bati.
Mama huyu nadai kuoteshwa na Mungu usiku wa kuamkia Machi 30 na leo ameanza kugawa dozi hiyo kwa gharama za sh. 200 tu kwa kipimo.
Mapema leo Mkuu wa Wilaya ya ya Morogoro, Said Mwambungu pamoja na maofisa wa wilaya akiwepo Mkaganga Mkuu wa Wilaya walifika nyumbani kwa mama huyo na kumwomba daktari achukue sampuli ya dawa hiyo kwa uchunguzi kujua usalama wake.
Zaidi ya watu 200 wanasadikiwa kupata huduma hiyo kwa siku mbili zilizopita.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu akizungumza jambo baada ya kutembelea eneo hilo la Kichangani na kuzungumza na Mama Fatma juu ya tiba yake na kumpa mwongozo wa kufanya shughjuli hiyo bila kuleta usumbufu wala madhara kwake na jamii itakayotumia tiba hiyo.
Mwambungu aliambatana na viongozi kadha wa ofisi yake baada ya kupata taarifa ya kuwapo kwa KIKOMBE katika Wilaya yake.
Hivi ndo Vikombe, Glasi na Bilauri zinazotumika kugawa dozi ya kutibu magonjwa mbalimbali yakiwapo yale sugu yaliyoshindikana kwa dawa za kisomi.
Aidha Mama fatma yeye alikuwa ni mtoa tiba Mbada tabgu mwanzoni mwa miaka ya tisini hadi hapo alipoooteshwa na Mungu.
Haya Watanzania huenda ndo yale mambo ya unabii yanayo semwa katika vitabu vitakatifu kuwa nyakati za mwisho.
0 comments:
Post a Comment