Nafasi Ya Matangazo

April 15, 2010

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma ya akinamama wa kabila la Wamasai mara tu alipowasiri kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro kuanza ziara ya siku tatu mkoani Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akiwakabidhi vifaa vya hospitali kwa ajili ya zahanati ya Ishinde wilayani Same. Wanaopokea vifaa hivyo ni mganga wa zahanati hiyo ndugu Ruth Mushi (kulia),akifuatiwa na mganga mkuu wa wilaya ya Same Dr. Zawadi Abdallah na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Monica Mbega.
Wananchi wakimsikiliza...alipokuwa akihutubia.NAAVACHEWE!!
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza Bibi Asha Mrutu anayeishi katika kijiji cha Ishinde,Wilayani Same mara baada ya kumkabidhi kadi ya uanachama wa Jumuia ya Umoja wa Wanawake,UWT. Bibi Asha alikuwa miongoni mwa wanawake 60 waliopewa kadi za UWT na mama Salma wakati alipozuru wilayani Same jana.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akifungua rasmi zahanati ya kijiji cha Ishinde kilichoko katika Wilaya ya Same,mkoani Kilimanjaro tarehe 14.4.2010. Wengine katika picha (kulia kwenda kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega,Mama Salma, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same Daktari Zawadi Kessy Abdallah na Mkuu wa Wilaya ya Same ndugu Marwa.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa jengo la Maabara ya fizikia, biolojia na kemia katika shule ya sekondari ya wasichana ya Joyland iliyopo mjini Same tarehe 14.4.2010. Wengine katika picha (kulia kwenda kushoto), ni Mkuu wa mkoa mheshimiwa Monica Mbega, Mkuu wa shule hiyo Sister Sylvestor Msaky,mama Salma, na Mkuu wa shirika la mapadre la maisha ya kitume ya kazi ya roho mtakatifu Padre Joseph Israel,(mmiliki wa shule hiyo).
Posted by MROKI On Thursday, April 15, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo