Jakaya Kikwete alisalimiana na ajuza Bibi Makihiyo Baluah (102) mkazi wa Korogwe Mkoani Tanga alipomtembelea bibi huyo nyumbani kwake mjini hivi karibuni .Bibi Baluah ni mke wa hayati Mzee Baluah ambaye alikuwa rafiki wa Baba wa JK , hayati Mzee Mrisho Kikwete.
a hebu tafuta kwenye maktaba yako picha ya mzee mkapa kwenye kigoda kama hiki ndani ya nyumba ya mbavu za mbwa, kikwete mtu bwana
ReplyDeletebinafsi sipendelei matumizi ya maneno kama Ajuza au Kikongwe. Ungesema bibit/mama wa miaka...
ReplyDeleteManeno Ajuza na Kikongwe yana negative connotation fulani. Kama vile huy mtu kakongoroka.
Na we anony wa hapo juu, yaani kusalimiana na huyu bibi ndio unampa shavu Kikwete? Ufisadi wake wote huooni? Tuache siasa za kishabiki. Sifia panapostahili sifa. Kumpa mtu mkono kitu gani kwani? Kwa siasa za Marekani wanaita hii photo-op (i.e. Photo oportunity). Anafanya hivi kujikweza kisiasa. Ina maana gani unakuja kumsalimia mtu nyumbani wakati ufisadi wa serikali yako unafanya maisha yake yazidi kuwa magumu siku baada ya siku
Ndugu zangu,
ReplyDeleteHii kitu anayofanya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika somo la Sociology au Mass Communication inajulikana kama GLITTERING GENERALITIES. Ni mtindo wa propaganda ambao unatumiwa kuamsha hisia kwamba kiongozi au mtu fulani mwenye mamlaka yu karibu na watu wa tabaka la chini.
Tofauti na mtu kama Mtawa Theresa wa Calcuta ambaye aliishi na kujuana na maskini, watu kama kina Marehemu Princess Diana au Prince Charles au William au hata Rais Kikwete na Mama Kikwete wanaweza kupiga picha wakiwa vijijini kwenye lindi la umasikini wakiteka maji kisimani kusaidia ujenzi wa shule. Au kama tunavyomuona Mheshimiwa Rais Kikwete kwenye picha hii akiwa na huyo ajuza masikini au zile picha zake akiwa kabeba beba watoto na kutembelea wagonjwa mahospitalini.
Kwa ufupi, ni kwamba hii propaganda strategy Mheshimiwa Rais Kikwete kwa sasa kaanza kuifuja kwa kuitumia mara kwa mara. Ili aendelee kutuamsha hisia abadilishe strategy halafu aanike ripoti ya madini na ya EPA na kuwafukuza na kuwapeleka wahusika mahakamani.