Nafasi Ya Matangazo

May 16, 2024











Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri Saba za mkoa huo kuhakikisha wanatatua changamoto na matatizo mbalimbali yanayowakabili Walimu katika maeneo yao ili kuongeza ari katika ufundishaji na ufaulu wa wanafunzi mashuleni.

Mkuu wa mkoa wa Singida ametoa maagizo hayo katika ufunguzi wa Kongamano la Siku Mbili la Walimu kutoka mikoa ya Kanda ya kati na Kaskazini ambao wamekutana mjini Singida kujadili masuala mbalimbali yanayoikabili sekta hiyo ikiwemo namna bora ya kutetea maslahi yao na kuweka mipango na mikakati madhubuti ya kuongeza maradufu ufundishaji na ufaulu katika kanda zao.

Mkuu huyo wa mkoa wa Singida amesisitiza kuwa matatizo mengi yanayowakabili walimu yanaweza kutatuliwa na Viongozi waliopo ngazi za wilaya kwa kukaa pamoja na kujadili kwa kina namna bora ya kutafuta majawabu sahihi ambayo yataongeza ari ya walimu kufundisha na kupandisha ufaulu kwa wanafunzi.

Amesema Serikali ya awamu ya Sita imefanya mambo makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ya sekta ya elimu hivyo ni muhimu kwa Walimu kote nchini kumuunga mkono Rais Dakta Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu mkubwa ili kutengeneza Wanafunzi bora ambao Watalisaidia Taifa kusonge mbele Kimaendeleo haraka.

Kuhusu maadili ya Wanafunzi, Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego amewahimiza Walimu kuhakikisha wanawalea wanafunzi katika njia sahihi kwa kuzingatia mila na Desturi za Kitanzania ili kuwaepusha na matatizo ya utovu wa nidhamu.

Halima Dendego amewataka walimu kutoa adhabu stahiki kwa wanafunzi wanaoenda kinyume na taratibu za shule kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo nchini ili kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza shule au vyuo wanakuwa na maadili mazuri yanayompendeza Mwenyezi Mungu na Taifa kwa ujumla.

Naye, Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Dkt Fatuma Mganga amewataka Walimu kuzingatia kanuni na taratibu katika malezi ya wanafunzi ili kukabiliana na tatizo la mimba kwa wanafunzi jambo ambalo amesema halipendezi hata kidogo.

Dkt Fatuma Mganga amewahimiza Walimu kuongeza bidii na ubunifu katika ufundishaji ili kuhakikisha Taifa la Tanzania linapata Watalaamu Wazuri ambao watasaidia nchi kusonga mbele kimaendeleo haraka.

Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania -CWT- Leah Ulaya ameiomba Serikali kuendelea kushughulikia matatizo yanayowakabili walimu ikiwemo ulipaji wa madeni na upandishaji wa vyeo kwa wakati jambo ambalo amesema litasaidia Walimu 
Posted by MROKI On Thursday, May 16, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo