Nafasi Ya Matangazo

May 15, 2024

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko  amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Michael Battle Sr. kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwamo matumizi ya vyanzo mbalimbali vya nishati ya umeme

Mazungumzo hayo yamefanyika  Mei 14, 2024 katika Ofisi ndogo za Wizara, Jijini Dar es Salaam,  ambapo viongozi hao wawili wamekubaliana  kuhusu umuhimu wa matumizi ya vyanzo mbadala vya umeme ikiwemo upepo, jotoardhi, jua na gesi asilia ikiwa njia mojawapo ya kuchagiza maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.

Dkt. Biteko amesema kuwa mahitaji ya nishati ya umeme nchini yamekuwa ya kiongezeka kwa kasi kufuatia   ukuaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi na maendeleo ya kijamii.
 

Posted by MROKI On Wednesday, May 15, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo