Nafasi Ya Matangazo

February 29, 2024

 

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaji Ali Hassan Mwinyi 'Mzee Ruksa' amefariki Dunia hii leo Februari 29,2024.

Taarifa ya kifo cha Mwinyi imetolewa Rais Samia Suluhu Hassan ambapo amesema Mwinyi amefikwa na umauti wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam.

Mwinyi aliyezaliwa Mei 8,1925 Mkuranga Mkoani Pwani alikuwa Rais wa pili wa Tanzania alichukua nafasi Novemba 5,1985 baada ya kung'atuka kwa baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere na alifikia ukomo wake Novemba 23, 1995.

Mzee Mwinyi atakumbukwa na wengi kutokana na Mfumo wake wa kiutawala uliofungua masoko huria na kupelekea kupachikwa jina la Mzee Ruksa. 
Februari 2,2024 familia yake ilitoa taarifa juu ya kulazwa kwa Mzee Mwinyi na kuwaomba watanzania kukuombea Dua.

Taarifa hiyo ilisema, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi  amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua. 

Anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari. 

Kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu. Hivyo Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala, na Maombi.

Posted by MROKI On Thursday, February 29, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo