Nafasi Ya Matangazo

September 18, 2023

 


Na John Mapepele 
Msanii maarufu duniani kwenye eneo la filamu kutoka nchini ambaye ana zaidi ya wafuasi milioni mia mbili katika mitandao  yake, Sanjay Dutt leo Septemba 18, 2023 ametua  kuanza Royal Tour hapa nchini.

Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na kupokewa na Mkurugenzi wa Utalii nchini Dkt. Thereza Mugobi na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Damasi Mfugale, bwana Dutt amesema ameamua kuja kutembelea vivutio vya utalii nchini kufuatia Filamu ya The Royal Tour iliyochezwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuonyesha hazina ya utajiri wa vivutio vya utalii nchini.

"Naipenda sana Tanzania, naiona niifanye Tanzania kuwa nyumba yangu ya pili sasa baada ya kuitazama filamu ya The Royal Tour" amesisitiza Dutt.

Aidha, amesema ameamua  kuwa balozi wa kujitolea kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia mitandao yake kutokana na mapenzi yake kwa Taifa la Tanzania.

Mkurugenzi wa Utalii nchini Dkt Thereza Mugobi amefafanua kuwa Tanzania imefarijika  kupata ugeni wa msanii huyo maarufu duniani kutoka  India eneo ambalo lina idadi kubwa ya watu takribani bilioni 1.4 ambao ni soko la kimkakati la Tanzania.

"Ujio wa Dutt ni faraja kwetu kwa vile tunatambua  itasaidia  kuwa vuta wageni wengi kutoka bara la Asia ambako yeye anawafuasi wengi" ameongeza Dkt. Mugobi.

Kwa upande wake  Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Damasi Mfugale amesema Serikali itaendelea  kuwakaribisha watu maarufu duniani ili wasaidie kufikia azma ya kufikisha wageni milioni tano ifikapo 2025 na kuliingizia Taifa dola bilioni  Sita za kimarekani.
Posted by MROKI On Monday, September 18, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo