Nafasi Ya Matangazo

June 06, 2023







Na Sixmund Begashe
Wizara ya Maliasili na Utalii imeipongeza Timu ya Yanga pamoja na Rais wa Yanga Eng. Said Helsie kwa kuendelea kuitangaza vyema nchi yetu Afrika na Duniani kwa kushika nafasi ya pili kwenye fainali za Kombe la Shirikisho Barani Afrika sambamba na kutoa mfungaji bora na golikipa bora wa mashindano hayo. 

Akizungumza kwenye kuhitimisha Hotuba yake ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na kwa Mwaka 2023/2024, Bungeni Jijini  Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa ameongeza kuwa hatua hiyo imewezesha Brandi ya Tanzania kuzidi kujulikana katika mataifa mbalimbali na hivyo kuchochea hamasa za watalii kutoka mataifa mbalimbali kuja kutembelea vivutio vyetu.

Waziri Mchengerwa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye kwa kujitoa kwake kupitia  filamu ya “Tanzania; The Royal” ilivyoleta mafanikio lukuki nchini  si tu watalii Kwa kuongezeka, lakini pia nchi  sasa ni kivutio cha mastaa mbalimbali na watu mashuhuri ambao wamekuwa wakija hapa nchini na wanaendelea kumiminika nchini.

Kutokana na Ushindi wa Timu ya Yanga, Wizara hiyo imetoa ofa kwa wachezaji na Viongozi wa Klabu ya  club hiyo, kutembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti na Hifadhi ya Ngorongoro wakati wa mapumziko yao. 

"Sambamba na hilo niwakaribishe pia mashabiki wote wa Yanga kwenda kujumuika pamoja na wachezaji hao katika safari hiyo katika tarehe itakayotangazwa na utaratibu utakaowekwa. Ziara hizo tunapendekeza iitwe, “The CAF Finalists Royal Tour.” Alisema Waziri Mchengerwa.

Bunge  limeidhinisha jumla ya Shilingi 654,668,208,000 kwa matumizi ya Fungu 69 - Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2023/2024, kati ya fedha hizo, Shilingi 486,501,449,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi 168,166,759,000 ni za miradi ya maendeleo.
Posted by MROKI On Tuesday, June 06, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo