Nafasi Ya Matangazo

May 28, 2023


Na Patricia Kimelemeta 
MAOfISA  Ustawi wa Jamii nchini wameagizwa  kushirikiana na watendaji wa Kata na Mtaa kutoa elimu kwa jamii ya kuwalinda watoto Ili wasiwese kufanyiwa vitendo vya ukatili Kwa sababu vinawarudisha nyuma Katika ukuaji wao.

Hata hivyo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee kutoka makundi maalum, Dk. Nandela Mhando amesema kuwa, kutokea kwa vitendo vya ukatili Katika jamii kunatokana na wazazi na walezi kutowajibika ipasavyo katika malezi ya watoto,Hali ambayo inawaathiri kimwili na kiakili.

Amesema kuwa, kutokana na Hali hiyo Maofisa hao wanapaswa  kushirikiana na watendaji wa kata na mtaa ili kupita nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kutoa elimu ya Malezi jumuishi kwa jamii na kila mmoja aweze kutambua umuhimu wake wa kuwalinda na kuwasimamia watoto ipasavyo jambo ambalo linaweza kupunguza vitendo vya ukatili.

" Watoto wanastairi kulindwa na jamii mzima, sio mzazi au mlezi peke yake, ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa mtoto anaishi katika mazingira salama Ili aweze kukua katika hali ya utimilifu,  hivyo basi  tunapaswa kukishirikiana na watendaji wa kata au mtaa pamoja na mamlaka nyingine Ili kupita nyumba kwa nyumba Ili kutoa elimu ya Malezi jumuishi kwa Watoto, " amesema Dk Mhando. 

Ameongeza kuwa, wanaotekeleza vitendo vya ukatili wanaishi kwenye jamii ambapo ndipo ukatili unapoanzia, hivyo basi wakipewa elimu wanaweza kubadilika na wale ambao watakaoidi hatua kali zitachululiwa dhidi Yao.

Amesema kuwa madhara ya kumfanyia mtoto ukatili ni makubwa Kwa sababu yanaharibu ukuaji wake na saikolojia, hivyo basi kila mmoja anapaswa kukemea hali hiyo.

"Watoto waliopitia kwenye ukatili wanaathirika kisaikolojia, hata ukuaji wake unarudi nyuma, kama jamii inapaswa kuwajibika na wale watakaobainika kuwafanyia ukatili watachukuliwa hatua  Kali za kisheria Ili iwe fundisho kwa wengine.

" Kuna kesi nyingi za ubakaji, ulawiti, utesaji wa watoto na hata kuwadhuru kwa namna Moja au nyingine zinaendelea kwenye mahakama mbalimbali nchini, lengo ni kuwachukulia hatua kali wale wanaofanya vitendo hivyo, lakini kama Serikali tutaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali Ili kutoa elimu ya Malezi jumuishi Kwa jamii zetu," amesema.

Amesema kuwa, kutokana na hali hiyo,  maofisa Ustawi wa Jamii wakishirikiana na wadau wengine kuleta mabadiriko katika jamii Kwa sababu Kila mmoja atakua balozi wa 
kupinga vitendo vya ukatili.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vituo vya Kulea Watoto wadogo na wa shule ya Awali (Uviwada) Mkoa wa Dar Es Salaam, Shukuru Mwakasege amesema kuwa, wazazi na walezi kushinda kutimiza wajibu wao kunasababisha watoto wengi wanapofika kwenye vituo vya kulea watoto ( Day Care) tayari wamefanyiwa ukatili wa aina Moja au nyingine.

"Watoto wanaofikishwa vituoni  baadhi yao wanakua tayari wameshafanyiwa  vitendo vya ukatili, tumejaribu kuwaita wazazi na kuzungumza nao lakini hawatoi ushirikiano," amesema Mwakasege.

Ameongeza kuwa, kesi nyingi zinamaliziaa kifamilia huku wahusika wanakua hawajachukupiwa hatua, hivyo basi ameiomba Serikali kushirikiana na wadau wa vituo hivyo Ili waweze kutoa taarifa za matukio hayo na wahusika wachukuliwe hatua kali.

" Vituo vyetu vinachukua watoto kuanzia umri wa miaka mitatu hadi mitano, lakini baadhi yao wanakuja wakiwa tayari  wamelawitiwa, wamebakwa au kuteswa kwa namna moja au nyingine, na wazazi wanaficha taarifa hizo, " amesema.

Amesema kuwa, kwakuwa vituo hivyo havina watalaam wa saikolojia, wanaendelea kukaa nao hao watoto bila ya kuwapa msaada wowote.

Ameiomba Serikali kutoa elimu kwa jamii Ili waweze kukomesha vitendo vya ukatili Kwa watoto.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wamesema kuwa, kutowajibika Kwa wazazi na walezi kwenye makuzi ya mtoto kunachangia kuendelea kujitokeza kwa vitendo vya ukatili.

" Serikali inapaswa kutunga Sheria kali za kuwachukulia wazazi na walezi wanaoshindqa kutimiza wajibu wao Katika malezi ya watoto, hali ambayo inasababisha kuendelea kujitokeza Kwa matukio ya ukatili," amesema Ashura Juma.

Takwimu zilizotolewa na serikali Mwaka Jana zinaonyesha kuwa  watoto wenye umri kuanzia miaka 0 hadi 19 walikadiriwa kuwa 31,040,164 ambao ni sawa na asilimia 53.85 ya watu wote nchini Tanzania.
Posted by MROKI On Sunday, May 28, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo