Nafasi Ya Matangazo

March 19, 2023

Na WAF - Kagera
NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel kwa niaba ya Waziri wa Afya amewaasa wananchi wa Mkoa wa Kagera kufuata maelekezo ya Wataalamu wa afya katika maeneo yao ili kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya mlipuko. 

Dkt. Mollel ametoa wito huo leo Machi 18, 2023 wakati akiongea na vyombo vya habari baada ya kufanya kikao na Wataalamu wa afya katika Mkoa huo ili kuona namna bora ya kupambana dhidi ya mlipuko ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko. 

"Tuendelee kuwaasa wananchi maelekezo yote ambayo Wataalamu wa afya wanayatoa mfano mambo ya kuzikana, hata kama mgonjwa hajaonesha dalili zinazofanana kama swala la maziko wayazingatie kwa Wataalamu na maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya." Amesema. 

Aidha, Dkt. Mollel ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa namna walivojitoa katika kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali tangu kuibuka kwa ugonjwa usiojulikana Machi 16, 2023 Mkoani hapo.

Sambamba na hilo amewapongeza Watumishi wa afya katika ngazi zote, kuanzia ngazi ya Mkoa mpaka ngazi ya zahanati kwa namna bora wanavoendelea kupambana katika utoaji huduma jambo ndio maana bali ya afya inaendelea kuimarika.

Pia, amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa pesa, vifaa, dawa na rasilimali watu ili kuhakikisha hali ya afya katika Mkoa wa Kagera inaimarika na utoaji huduma unakuwa bora.
Posted by MROKI On Sunday, March 19, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo