Nafasi Ya Matangazo

August 03, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya siku moja nchini tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati Nyimbo za Taifa (Tanzania na Zambia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wakisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kwenye mapokezi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili na matarumbeta vilivyokuwa vikitoa burudani wakati wa mapokezi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wa mapokezi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanahabari katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpatia maelezo kuhusu picha na vitabu vya Kiswahili mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema na baadae kukabidhi zawadi hizo katika ziara yake ya siku moja nchini kabla ya kuanza mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpatia maelezo kuhusu picha na vitabu vya Kiswahili mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema na baadae kukabidhi zawadi hizo katika ziara yake ya siku moja nchini kabla ya kuanza mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema
***************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia.
 
Makubaliano hayo ni pamoja na ushirikiano katika masuala ya miundombinu ya reli kwa kutafuta fedha kwa pamoja ili kuimarisha reli ya TAZARA kwa kiwango cha SGR.
 
Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kiserikali ya siku moja ya Rais Hichilema nchini Tanzania.
 
Pia Marais hao wamejadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wadogo wadogo ikiwemo vikwazo vya kikodi na vibali vya kuingia nchi hizo mbili kwa ajili ya biashara.  
 
Masuala mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na nishati, kilimo, ulinzi, kufufua Tume inayojadili mahusiano ya nchi mbili na namna ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
 
Wakati huo huo, Rais Samia na Rais Hichilema wameshuhudia utiaji saini wa mikataba mitatu kati ya Tanzania na Zambia kwenye sekta ya ulinzi, utamaduni na sanaa.
 
Rais Samia ameagana na mgeni wake Rais Hichilema katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam mara baada ya kukamilisha ziara yake.
 
Posted by MROKI On Wednesday, August 03, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo