Nafasi Ya Matangazo

February 07, 2017


Bunge jana liliketi kikao chake cha sita katika mkutano wa Sita wa Bunge la 11 mjini Dodoma. Mbali na kipindi cha Maswali na majibu lakini pia Wabunge walipokea taarifa za Kamati mbili za Kudumu za Bunge ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya na Ile ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Pichani juu ni Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdul Aziz Abood akiuliza swali Bungeni Mjini Dodoma jana kuhusiana na masuala ya usambazaji umeme katika baadhi ya vijiji klatika jimbo lake.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano Mh. Luhaga Mpina akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma ambayo yalielekezwa katika Wizara yake.
 Mbunge wa Konde Zanzibar, Khatib Said Haji akiuliza swali kwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Bungeni mjini Dodoma jana juu ya masuala ya ucheleweshaji wa kesi mbalimbali kutokana na ucheleweshaji wa upelelezi jambo linalosababisha kuwepo na ongezeko kubwa la mahabusu Magerezani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akijibu swali la Mbunge wa Konde Khatib Said Haji pamoja na maswali mengine ya nyongeza.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harison Mwakyembe akisaidia kujibu maswali yaliyoelekezwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambayo yalihitaji ufafanuzi wa kina wa kisheria na hasa pale yalipozungumza mambo yanayohusiana na Ugaidi.
 Mbunge wa Viti Maalum, Pauline Gekul akiuliza swali Bungeni.
 Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati akiuliza swali Bungeni.
 Wabunge wakifuatilia mjadala wa Bunge mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani akijibu maswali yaliyoulizwa katika Wizara yake.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medad Kalemani (kulia) akizungumza jana na Mbunge wa Morogoro Mjini Bungeni mjini Dodoma 
 
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Kagera,  Oliver  Semuguruka Bungeni mjini Dodoma

 Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson akizungumza na Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby Bungeni mjini

 Wabunge mbalimbali wakichangia mijada ya kamati.
 Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako akijibu hoja.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akijibu hoja zilizoibuliwa na Wabunge wa katika wa Mjadala wa taarifa za kamati.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza Bungeni.
Baada ya kuugua kwa Muda Mrefu Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani 'Maji Marefu' (kulia) aliwasili Bungeni jana na kulakiwa na Wabunge wenzake kwa furaha.
 Wabunge wakiwasili Bungeni
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiongozana na kuzungumza na Mbunge wa Kuteuliwa na Rais Abdallah Bulembo.
 Mbunge akiwasili Bungeni
Wabunge wakizungumza nje ya Bunge.
Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara akizungumza na Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
Posted by MROKI On Tuesday, February 07, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo