Nafasi Ya Matangazo

May 30, 2016

Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo,akiongea na baadhi ya  wazazi wa watoto wanaosoma katika shule mbalimbali waliofika kwenye  viwanja vya TTCL Kijitonyama  jijini Dar es Salaam, wakati wa madhimisho ya siku ya hedhi  Salama  mwishoni mwa wiki.

Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo,akiwagawia kinywaji cha Grand Malt  baadhi ya  wazazi wa watoto wanaosoma katika shule mbalimbali waliofika kwenye  viwanja vya TTCL Kijitonyama  jijini Dar es Salaam, wakati wa madhimisho ya siku ya hedhi  Salama  mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wanafunzi wa kike wakimsikiliza  Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo wakati wa maadhimisho hayo.
***********

MENEJA Uhusiano wa nje wa kampuni ya TBL Group,Emma Oriyo, amesema kuwa jukumu la kuwainua watoto wa kike nchini sio la serikali bali linamhusu kila mtanzania ikiwemo makampuni,taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi duniani iliyoadhimishwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ,alisema kuwa siku hiyo ni muhimu kuadhimishwa kwa kuwa inatukumbusha watanzania kutofumbia matatizo yaliyopo kwenye jamii yetu na kuangalia  namna ya kuyashughulikia.

“Hapa Tanzania Changamoto za hedhi kwa watoto wa kike ni kubwa wengi wakiwa wanakosa vifaa vya kuwaweka salama pia shule nyingi hazina miuondombinu rafiki kwa wasichana kujiweka salama wanapokuwa kwenye hedhi,matokeo yake wengi wanakuwa hawahudhuri masomo na kujikuta wamebaki nyuma ya wenzao wa kiume”.Alisema.

Amesema TBL Group katika miradi yake ya afya ya kusaidia jamii imeanza kuliangalia suala hili kwa undani ili kuweza kushirikiana na wadau wengine kukabiliana nalo “Leo kampuni yetu ni moja ya wadhamini wa tukio hili la siku ya hedhi ambalo lengo lake kubwa ni kuelimisha jamii umuhimu wa kuungana kuondoa changamoto na hedhi na tutaendelea na jitihada hizi na kutekeleza  miradi mingine ya kusaidia kuboresha afya  nchini”.Alisema.

Alisema  watanzania wakiungana na serikali katika  kukabiliana na changamoto hizi  hali itakuwa nzuri na watoto wa kike kusoma katika mazingira mazuri na itapelekea wafanye vizuri kwenye masomo yao sambamba na wenzao wa kiume.

Emma alisema kuwa hali ya kukosa vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi na miundombinu isiyo rafiki mashuleni mbali na utoro mashuleni pia inawasabishia watoto  wa kike kutojiamini na wakikua bila kujiamini wanakuwa hawawezi kutoa maamuzi sahihi.

“Wadau wote tukiungana katika suala hili tutaweza kutekeleza dira ya maendeleo ya taifa ambayo kwa upande wa elimu ina kauli mbiu isemayo Elimu Bora bila ubaguzi inawezekana.Timiza wajibu wako”
Posted by MROKI On Monday, May 30, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo