Nafasi Ya Matangazo

November 17, 2015

Rais Dk John Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo katika ofisi za Ubalozi wa Ufaransa nchini kufuatia mauaji ya watu 132 kutoka mataifa mbalimbali yaliyofanywa na magaidi katika mji wa Paris, Ufaransa hivi karibuni. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak. Rais Magufuli alisaini kitabo hicho Dar es Salaam leo.
 Rais Dk John Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo katika ofisi za Ubalozi wa Ufaransa nchini kufuatia mauaji ya watu 132 kutoka mataifa mbalimbali yaliyofanywa na magaidi katika mji wa Paris, Ufaransa hivi karibuni.
 Rais Dk John Magufuli akimkabidhi Balozi Ufaransa nchini, Malika Berak  barua ya salamu za maombolezo bakitia baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ofisi za Ubalozi wa Ufaransa nchini kufuatia mauaji ya watu 132 kutoka mataifa mbalimbali yaliyofanywa na magaidi katika mji wa Paris, Ufaransa hivi karibuni.
 Rais Dk John Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufarasa nchini, Malika Berak na kumpa pole.
 Rais Magufuli akiwa na watumishi wa ubalozi huo
Rais Dk Magufuli akiagana na Balozi wa Ufaransa.
************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya watu zaidi 130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana na mashambulizi ya ugaidi mjini Paris, Ufaransa.

Pamoja na kutia saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande na kumuombea uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu.

Dk.Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak amesema Tanzania imeguswa na vifo hivyo na inaungana na Ufaransa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Aidha Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili waweze kuungan a na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amewasili Mjini Dodoma jioni hii kwa shughuli mbalimbali za kikazi.

Mheshimiwa Magufuli amesafiri kwa gari kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na taarifa ya shughuli atakazozifanya mtaarifiwa baadaye.
Posted by MROKI On Tuesday, November 17, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo