Nafasi Ya Matangazo

July 18, 2015

Kikosi cha Yanga ambacho leo kimekubali kichapo cha bao 2-1 na Gor-Mahia ya Kenya.
Wababe wa Yanga timu ya Gor-Mahia
Mchezaji wa Yanga, Amis Tambwe akiwa chini huku wachezaji Collins Okoth (kulia) na Harun Shakava (kushoto) wa Gor Mahia ya Kenya wakiwania mpira wakati wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Kagame uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Yanga imefungwa mabao 2-1.
DAKIKA 92 za mchezo rasmi wa ufunguzi wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashriki 'Kagame Cup 2015' zimemaliza huku zikiwaacha Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga na maumivuvu ya kichapo cha mabao 2-1 dhdi ya Gormahia ya Kenya.

Yanga ndio walikuwa wakanzwa kupata bao katika dakika 4  baada ya mlinzi wa nyuma wa Gormahia kujifunga lakini dakika  12 baadae wakasawazisha kupitia Harun Shakav.

Yanga walicheza wakiwa pungufu baada ya mshambuliaji wake Mzimbabwe, Donald Ngoma kulambwa kadi mbili za njano zilizozaa nyekundu na akatolewa nje katika dakika ya 24.

Yanga itajilaumu baada ya nahodha wake kukosa penati katika dakika 17 kufutia adhabu baada ya mchezajio wa Gor Mahia kuunawa mpira eneo la hatari.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam timu ya APR ya Rwanda imeanza vyema  safari ya kulitaka kombe hilo linalodhaminiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Shandy ya Sudan. goli lilofungwa na  kiungo Bizimana Djihad, dakika ya 64.

Aidha katika uwanja wa Karume palikuwa na mchezo mwingine uliowakutanisha KMKM kutoka Visiwani Zanzibar na Telecom ya Dijbout. 
Posted by MROKI On Saturday, July 18, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo